Quantcast
Channel: MRISHO'S BLOG
Viewing all 4405 articles
Browse latest View live

taarifa kwa umma kuhusu dawa bandia

$
0
0
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZILIZOTOLEWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO JUU YA KUINGIZWA NA KUWEPO KWA DAWA BANDIA ZA KUTIBU KIFUA KIKUU

1.  Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini na mitandao ya kimataifa imetoa taarifa juu ya kuingizwa au kuwepo kwa dawa za kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (Tuberculosis – TB) zinazohisiwa kuwa ni bandia katika baadhi ya nchi za bara la Afrika ikiwemo Tanzania.

2.   Taarifa zilizotolewa zimeainisha kuwa sampuli zilichukuliwa kutoka kwenye maduka ya dawa binafsi (private pharmacies). Ufafanuzi unatolewa kwamba, dawa za TB huingizwa nchini kwa utaratibu maalum ambapo ni Bohari ya Dawa (MSD) pekee ndiyo hununua na kusambaza dawa hizi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali na baadhi ya vituo binafsi chini ya kibali na usimamizi maalum. Dawa zinazoruhusiwa kuingia nchini ni zile zilizosajiliwa na kuthibitishwa na TFDA. Dawa za kutibu TB haziruhusiwi kuuzwa kwenye maduka ya dawa binafsi.

3.      TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuwa taarifa hizo sio za kweli. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mifumo ya ufuatiliaji wa ubora na usalama wa dawa ingeweza kubaini dawa hizo katika soko.  Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu zilizopo, matoleo (batches) 89 ya dawa za TB yaliyochukuliwa kwenye vituo vya forodha (ports of entry) kati ya Januari 2011 na Disemba 2012 na kupimwa kwenye Maabara ya TFDA yameonesha kukidhi vipimo vya Maabara.  Aidha, matoleo 46 ya dawa za TB yaliyochukuliwa kutoka katika vituo vya afya vya Serikali kati ya Juni – Disemba 2012 pia yamekidhi vipimo vya Maabara baada ya kuchunguzwa.

4.      TFDA imeweka mifumo thabiti ya kusajili, kukagua, kuchunguza kwenye Maabara na kufuatilia ubora wa dawa zilizoko kwenye soko. Kupitia mifumo hii, TFDA inaweza kubaini uwepo wa dawa duni na bandia katika soko. Pamoja na mifumo iliyopo, TFDA inawaomba wananchi kutoa taarifa pale wanapokuwa na mashaka kuhusu ubora na usalama wa  dawa za TB  pamoja na dawa nyingine ili hatua stahili zichukuliwe kwa mujibu wa sheria. 

5.      Mamlaka inawashauri wagonjwa wa TB kuendelea kutumia dawa za kutibu ugonjwa huo zinazotolewa bure kwenye vituo vya afya vilivyoruhusiwa na Serikali kwa kuwa ni bora, salama na zenye ufanisi uliothibitishwa na TFDA.

6.      TFDA itaendelea kufuatilia taarifa hizo na kufanya ukaguzi zaidi ili kuhakikisha kwamba dawa za TB zinazotumika nchini ni bora na salama wakati wote.
Kwa maelezo au ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na;

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),
S.L.P 77150, Dar Es Salaam
Simu: +255 22 2452108/22 2450512
Au:  0658 445222/ 0685 701735/ 0777 700002
Nukushi: +255 22 2450793
Barua pepe: info@tfda.or.tz, Tovuti: www.tfda.or.tz

Skylight Band kukinukisha Valentine's Day New Maisha Club kesho

Mkutano wa tatu wa wadau wa NSSF waanza rasmi leo jijini Arusha

$
0
0
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akizungumza na kuzindua wimbo maalum wa NSSF uliotungwa na Wasanii hapa nchini wajiitao All Stars,mbele ya wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akifafanua jambo kwa umakini  mbele ya  Wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akifafanua jambo mapema leo asubuhi wakati mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,ukiendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Meneja wa kanda na anaeshughulikia Idara mbalimbali za serikali kutoka NSSF,Rehema Chuma akifafanua namna ya uendeshaji wa shirika hilo kwa  wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akichangia moja ya mada zilizokuwa sikitolewa kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia akichangia moja ya mada zilizokuwa sikitolewa kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 
Mmoja wa wajumbe wa NSSF,Peter Sumbi aliyekuwa akifanya kazi shirika la Wildlife Fund akitoa ushuhuda wake,namna alivyopata ajali na kufanikiwa kupata fao lake la ajali kazini kutoka kwa shirika la NSSF na hatimaye kufaidi matunda kupitia mfuko huo.
Pichani ni Mwenyekiti wa wasataafu wa TAZARA,Injinia Mwl.Sango akitoa ushuhuda wake kuhusiana na namna shirika la NSSF lilivyowasaidia wastaafu wa shirika la TAZARA,kupitia mfuko wa pensheni na fao la kujitoa.
Sehemu ya Meza kuu ya mkutano huo.
Sehemu ya Wabunge waliopo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mifuko ya Jamii nchini wakiwa kwenye mkutanohuo.
 Baadhi ya watendaji wakuu wa NSSF wakiwa mkutanoni.
 Meneja Mahusiano wa PPF,Lulu Mengele na  Meneja Mahusiano wa SSRA,Sarah Kibonde wakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano huo unaoendelea hivi sasa.
 Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA),Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiwa sambamba na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nasari (CHADEMA) na Wadau wengine wakifuatilia yanayojiri hivi sana kwenye mkutano wa NSSF.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano wa NSS unaoendelea hivi sana ndani ya ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
 Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mkoani  Njombe,Mh. Deo Filikunjombe (CCM) akiwa na baadhi ya Wabunge Wenzake wanaohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo ambao umewakutanisha wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali jijini Arusha.
Mwenyekiti wa kikao cha awamu ya kwanza cha Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Daudi Msangi akitoa utaratibu kwa Wanachama na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unaoendelea ,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza jambo na  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori mapema leo asubuhi kabla ya kuanza kwa mkutano wa shirika hilo.
Wadau.
 Mkutano ukiendelea. 

Picha zote na Othman Michuzi

KALUNDE BAND KUSHEREHEKEA MIAKA SABA YA KUZALIWA KWAKE SIKU YA WAPENDANAO

$
0
0
Watu mbalimbali wako katika hekaheka ya kusherehekea siku ya wapendanao maarufu kama Valentine’s Day. Lakini KALUNDE BAND inajiunga katika sherehe hiyo ikiwa na sababu ya ziada kuserebuka na kuserebusha mashabiki wake katika siku hii kwa onesho maalumu  litalofanyika Alhamisi siku ya Valentine pale katika kiota cha maraha cha wapendanao cha Trinity maeneo ya  Oysterbay jijini Dar es salaamkaribu na Ubalozi wa Uganda  kuanzia  Saa 1:00  jioni na kuendelea hadi saa 6:00 usiku.

Siku ya Valentine ni muhimu kwa Kalunde kwani ndiyo siku ambayo bandhii  ilianzishwa. Band ilianzishwa tarehe 14.02.2006.

Kukupa burudani hiyo ya kuadhimisha siku ya wapendanao sambamba na HAPPY BIRTHDYA ya kutimiza miaka saba kamili ya KALUNDE BAND ni kundi zima la bendi hiyo kama ifuatavyo.

Deo Mwanambilimbi - Rais wa Band - Muasisi wa Band
Debora Nyangi - Meneja - Muasisi
Bob Rudala - Kiongozi wa wanamuziki
Bony Kaprobo - Solo Guitar - Band Stage Leader
Shehe Mwakichui - Keyboard Player / Mwimbaji - Muasisi wa band
Edson Allen (Eddy) - Solo Guitar
Othman Amri Majuto - Bass Guitar
Rajab Nyunyusa - Tumba
Alfa - Drummer
Mackie Fanta - Mwimbaji
Devotha, Mwapwani Yahya, Shila, Amina, wote hawa ni waimbaji


ENEO : TRINITY OYSTERBAY KARIBU NA UBALOZI WA UGANDA

KIINGILIO: Tsh. 5,000.00

GETINI : ZAWADI NI GLASS OF WINE AU SHAMPEIN

MUDA: SAA 1:00 JIONI - SAA 6:00 USIKU

PIA COUPLE ITAKAYOPENDEZA WATAPEWA ZAWADI MAALUM USIKU HUO.
RAIS WA BENDI YA KALUNDE DEO MWANAMBILIMBI AKIONGOZA MASHAMBULIZI KATIKA MAONESHO MBALIMBALI



--

KALUNDE BAND YASHEREHEKEA VALENTINE KWA KISHINDO

$
0
0
1 
Mkurugenzi wa Bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiimba huku wacheza shoo wa bendi hiyo Kushoto ni Queen Vero na kulia ni Frola Bamboocha wakati wa onesho la Valentine lililofanyika kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu, Katika Onesho hilo pia bendi ya Kalunde imetimiza miaka 7 toka ianzishwa na kusherehekea mwaka wake wa saba wa utendaji wa kazi.
2 
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi kushoto Debora Nyangi Meneja wa bendi hiyo pamoja na Mwapwani mwimbaji wa bendi ya Kalunde kwa pamoja wakikata keki kuashiria sherehe za kutimiza miaka saba toka bendi hiyo ianzishwe.
3 
Meneja wa Bendi la Kalude Debora Nyangi akimlisha keki Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi katika onesho la Valentine na sherehe za utimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
4 
5 
Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi akimlisha keki Meneja wa Bendi la Kalude Debora Nyangi katika onesho la Valentine na sherehe za utimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
6 
Debora Nyangi akimlisha keki Shekh Mwakichui mwimbaji na mpiga kinanda wa bendi ya hiyo
7 
Debora Nyangi akimlisha keki Bon Kamprobo mpiga gitaa la solo maarufu wa bendi hiyo
8 
Debora Nyangi akimlisha keki Bob Ludala mmoja wa waimbaji maarufu na makini wa bendi ya Kalunde.
9 
Debora Nyangi akimlisha keki Eric mmoja wa mashabiki na wadau muhimu wa bendi ya Kalunde.
10
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiwa katika picha ya pamoja na Debora Nyangi ambaye pia ni Meneja wa bendi ya Kalunde na pia wakiwa wanamuziki waanzilishi wa bendi wakiwa pamoja na Deo Mwanambilimbi mwenyewe.
11 
Mashabiki wa bendi ya Kalunde wakijimwaga stejini wakati bendi hiyo ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu.
12 
Hapa ni Full Kushwangweka na Valentine kama wanavyoonekana katika picha mashabiki hawa wakiwa stejini.
13 
Mnenguaji Frola Bamboocha akijimwaga na mmoja wa mashabiki wa bendi ya kalunde kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay usiku huu.
14 
Hapa ni Burudani tu kama wanavyoonekana mashabiki hawa wa Kalunde Band.
15 
Bamboocha na Shabiki wake hapa ni Full Mzuka hebu wacheki.

Ongea na Janet yashow love na watoto wa KIWOHEDE Valentines Day.

$
0
0
Mwendeshaji wa Kipindi cha Ongea na Janet kinachorusshwa na Clouds Tv na DStv Channel 158 Bi. Janet Sosthenes Mwenda akisaini daftari la wageni katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwa ajili kufurahi na watoto hao katika sikukuu ya wapendanao pamoja na kukabidhi msaada.
Bi. Janet Sosthenes Mwenda akijaribu na kununua moja ya bidhaa za mikono zinazotengenezwa na watoto wa kituo cha Kiwohede. Kushoto Mratibu Mipango wa Kituo hicho Bi. Stella Mwambenja.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha Kiwohede Bi. Justa Mwaituka akizungumza na Mtangazaji wa Kipindi cha Ongea na Janet pamoja Crew nzima inayotengeneza kipindi hicho kuhusiana na maendeleo yaliyokwisha fikiwa mpaka sasa na mipango ya baadae ya kuboresha mazingira ya kituo hicho.
Mtangazaji wa kipindi cha Ongea na Janet na crew yake wakiimbia na kufurahi pamoja na watoto wa kituo cha Kiwohede siku ya Valentines.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho akitambulisha wageni kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa na kituo hapo akitoa shukrani kwa Bi. Janet Sosthenes Mwenda pamoja na Crew kwa kuonyesha upendo wa dhati kitu ambacho ni adimu kwao kutokana na mazingira waliyotoka.
Mtangazaji wa Kipindi cha Ongea na Janet akizungumza na watoto wa kituo cha Kiwohede ambapo amewataka kudumisha upendo baina yao na kujiona kama watu wengine, pia amewaasa kukazania elimu ambayo itawakomboa na kuweza kuwa kama yeye hapo baadae na amewaahidi kuendelea kuwa nao pamoja.
Janet Sosthenes Mwenda na Crew nzima ya Ongea na Janet wakikabidhi msaada wa fedha taslim Shilingi laki 5 kwa mwakilishi wa watoto hao ikiwa ni upendo wake katika siku hii ya wapendanao.
Baadhi ya Watoto wa kituo cha Kiwohede wakifurahia msaada huo kutoka kwa kipindi cha Ongea na Janet.
Crew nzima ya Ongea na Janet katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Kiwohede.
Janet Sosthenes Mwenda akishow love na Mkurugenzi Mkuu wa shirikila lisilo la kiserikali la Kiwohede Bi. Justa Mwaituka.

Goldie's husband, Andrew Harvey, opens up about the late singer

$
0
0

Goldie's husband opened up to Thenetng.com. Read the interview below...
When did you wed her? And were you still married as at when she passed yesterday?
We wed in December 2005 and were very much married when she passed indeed I was talking to her on arrival in Lagos before the fateful event
I see you moved back to England. Do you have another family?
I work in Malaysia, we have a private home in UK, I do not have a second family
Also did you have kids together?
No kids, we were planning this year
There had been speculation for many years that she was married to an ‘oyinbo’ man. But no one could lay hands on anything. Why did you keep it a ‘secret’? 
Our private life is nothing to do with work life, there has to be a balance
See more after the cut...


How did you hear of her death? I found out you last saw her in December?
I was talking to her on arrival in Lagos before the fateful event

How did you meet her? She must have been very young…
I met her at a friend’s leaving party and fell in love straight away, but had to work hard to persuade her I was genuine

So you will be planning to come here for burial rites…
Yes I have applied for visa and shall come next week

But how did you manage the Prezzo drama? 

Prezzo was part of BBA game, just like in the movies, there was nothing to fear

But funny it dragged way beyond BBA
It dragged because the media dragged it, other wise it would have died naturally. Prezzo will say anything to get attention

Do you think he fell in love? And did you ever think Susan liked him for a minute…?
People fall in love and it’s not impossible to love more than one person, but there are different levels. She liked him initially, but began to despise him and distanced herself as he tried to use her she complained he was very manipulative

How did you come about your alias ‘Oyibopeppay?
Oyiiibopeppay is a name used in the villages for white man getting burned in the sun. I used to work in the bush erecting BTS for MTN and Glo


You have direct access to her password? The memories album was posted on her twitter. Or you requested for an admin to post?
I am an official admin. I don’t need any password but my own. It was authorised by Goldie

One last question: so much speculation on cause of death. I see from your facebook timeline that you’ve followed the reports. Have the doctors/family/label told you what the cause of death is?
An autopsy is being carried out and we will await results. The rest is speculation and hearsay

And did she have any medical condition?
She had no medical condition,

Is it true she was in India recently?
She was in Malaysia, we spent Christmas together away from prying eyes

What will you miss most about her?
Everything, she was the most beautiful person I ever met, no moment was wasted. Sweet, intelligent, sexy and a magnificent cook!!!!

And she was a determined young lady…
Very. That’s what I liked about her

Are you originally from England? Was she officially a citizen of your country by marriage? Or that was not concluded?
I’m from England and was processing Nigerian citizenship before I was transferred to Malaysia. Of course she was citizen of UK before we met, she lived and schooled there

She was indeed a star, as I’m sure you’ve seen from the tributes coming from far and near. Even the BBC and Billboard recognise her star
Yes we saw it on BBC news tonight. It is a devastating loss, but I support just as much wherever she has gone to.

Skylight Band yakinukisha Valentines Day katika ukumbi wa New Maisha Club jijini Dar.

$
0
0
Kundi la Skylight Band likicheza sebene kwa style ya aina yake walipopiga show ya kukata shoka usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Maisha Club.
Rappa Joniko Flower akiimba huku akishow love na familia ya Skylight Band katika usiku wa wapendanao uliofanyika katika ukumbi wa New Maisha Club.
Mashabiki wapya wa Skylight Band wakishow love katika siku ya wapendao kwenye ukumbi wa New Maisha Club.
Mtasha akishow love na wadau.
Ama kweli duniani wawili wawili.... Mdogo wake Baloteli wa Bongo huyu hapa.
Uzao wa Bongo Star Search Mary Lukas na Salma Yusuf.

KUMBUKUMBU-SALAMU KWA BABA YETU KIPENZI.

$
0
0
Kazi ya Mungu haina makosa, lakini kwetu ni majonzi makubwa.
Kama binadamu tungekuwa na uwezo wa kukata rufaa ya kifo, hakika nasi tungekata rufaa mbele ya Mungu ili turudishiwe  baba yetu kipenzi, Geoffrey Nkurlu, na kuendelea kuishi pamoja nae hapa duniani.

Hakika,tunajikuta tukiandika barua hii kwa uchungu mkubwa, maana familia yako inaadhimisha miaka 12 ya kukukosa kwako, tangu  hapo tarehe kama ya leo 17/2/2001 ulipotutoka na kuwa mbali na sisi.

Baba mpendwa, watoto wako wote bado tumeshikamana  kwa pamoja kama jinsi wewe ulivyotulea na kutusisitiza  tuwe wamoja. Tuko pamoja katika dhiki na faraja,hakika tunaendelea kukuwaza, kukukumbuka, kukuenzi na kuishi katika maadili bora  ambayo ulitufunza.Kwa kweli tunakulilia miaka yote, maana mchango wako ni mkubwa katika kuilea familia yako, ambayo leo hii imeweza kusimama imara kutokana na malezi mema na  mapenzi yako.

Baba mpendwa, sisi watoto  wako, wakati mwingine kila tunapokufikiria, hakika mioyo yetu inashindwa kuamini kama ni kweli haupo pamoja nasi. Tangu kuzaliwa kwetu, umeweza kutulea, kutusumbukia na kutusomesha kwa kidogo chako ulichokuwa unakipata.

Kitendo kama hicho ni cha kipekee. Nani kama wewe? Maisha yetu bila wewe, yangekuwaje katika kipindi cha maisha yetu, tangu kuzaliwa kwetu, kukua na kufikia katika kila kipindi kigumu ambacho daima ni picha kamili ya maisha yetu.

Ingawa tupo mbali na wewe, lakini  umetutoka kimwili tu, kiroho tuko na wewe. Bado tunakumbuka kauli zako, ushauri wako katika familia yako uliyoiacha katika wasiwasi mkubwa. Tumelia sana. Tumeumia sana.Na tuonapo baba wa wenzetu wakifurahia na kupata hata mawaidha, nasi huwa tunaukumbuka uwepo wako.

Picha na mtiririko wa maisha yako ni ushahidi kuwa wewe ulikuwa baba bora kwetu, huku tukiamini Mungu muweza na muumba wa yote ataitumia fursa hiyo kama sehemu ya kukulaza mahali pema kwa unyenyekevu wako.

Suala zima la kifo, linaashiria kuwa ni sehemu ya mpito katika maisha ya duniani. Vitabu vyote vya dini vimekitaja kifo kuwa hakuna kiumbe ambaye anaweza kuvuka bila kupitia katika hatua hiyo, hivyo tunatumia nafasi hii kukuombea mwanga wa milele ukuangazie.

Baba mpendwa, wakati tunaendelea kuyakumbuka mazuri yako katika familia hii uliyoiacha hali ya kuwa bado inakuhitaji, macho yetu yanashindwa kuhimili mtiririko wa machozi katika mboni zetu, yakiwa ni mapenzi makubwa baina yako na yetu.

Kazi ya Mungu haina makosa, lakini kwa upande wako ni ngumu mno kukubali matokeo na kujua kweli hatutakuwa wote katika kipindi cha maisha ya duniani. Umetangulia baba. Jina la bwana libarikiwe,sisi tunaendelea kukulilia miaka yote.

Tusingeweza na hatukuwa na sababu ya kuzuia hitaji la Mungu. Ingawa sisi tulikupenda na kukuhitaji sana, lakini Mungu alikupenda zaidi na aliona muda wako wa kuishi duniani umekoma na hakika ulistahili kwenda kwake kwa mapenzi yake, kwa vile kifo ni njia yetu sote na  kila nafsi itaonja mauti. Dunia tunapita.

Sisi watoto wako,Masala,Matina,Nzigia,Amani,Angaza na Atuza.
Tunakulilia na kukuombea daima.

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki Me

$
0
0
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (left) greets the former government minister Basil Mramba during the meeting. 
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (left) greets the former government minister Basil Mramba during the meeting
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (with mic) addressing tourism stakeholders in Arusha.
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (with mic) addressing tourism stakeholders in Arusha
Director of Tanzania Tourist Board Dr. Aloyce Nzuki (right) paying attention to some of the tourism stakeholders during the meeting.
Director of Tanzania Tourist Board Dr. Aloyce Nzuki (right) paying attention to some of the tourism stakeholders during the meeting
Former Minister Basil Mramba talking to TANAPA officials Dr. Ezekiel Dembe, Acting Director of Touris_ (second left)_ Johnson Manase, Tourism Manager and Alphonce Akarrow, CIA(1)
Former Minister Basil Mramba talking to TANAPA officials Dr. Ezekiel Dembe, Acting Director of Touris; (second left); Johnson Manase, Tourism Manager and Alphonce Akarrow, CIA
Minister for Natural Resources Hon. Ambassador Khamis Kagasheki in a jovial mood with the CEO of Leopard Tours Mr. Fazal 
Minister for Natural Resources Hon. Ambassador Khamis Kagasheki in a jovial mood with the CEO of Leopard Tours Mr. Fazal
NCAA Public Relations Manager Adam Akyoo (right) talking to Paul Srakikya (middle) who is the Assistant Director of Ant poaching in the Ministry. 
NCAA Public Relations Manager Adam Akyoo (right) talking to Paul Srakikya (middle) who is the Assistant Director of Ant poaching in the Ministry
TANAPA representatives at the stakeholders meeting.
Tourism Stakeholders in the country listening attentively to the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki
TTB Managing Director Dr. Aloyce Nzuki and Kibo Palace Hotel Marketing Manager Charity Githinji were also there to attend Tourism Stakeholders meeting. 
TTB Managing Director Dr. Aloyce Nzuki and Kibo Palace Hotel Marketing Manager Charity Githinji were also there to attend Tourism Stakeholders meeting

WanaCCM Gongo la Mboto wampongeza Jerry Silaa kwa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu

$
0
0

Baadhi ya kinamama wa Gongo la Mboto ambao ni wananchama wa CCM wakiwasili kwenye Uwanja uliopo karibu na reli Gongo la Mboto katika mkutano wa hadhara wa kumpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na waendesha Boda boda wa Gongo la Mboto waliofika kumlaki akitokea mjini Dodoma.
Msafara wa waendesha Boda boda ukimsindikiza Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa kwenye viwanja vya Gongo la Mboto alipoandaliwa sherehe ya kumpongeza iliyoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
Watoto waliokuwa pembezoni mwa barabara wakimpungua kwa furaha Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa alipokuwa akipita na msafara wake.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya viongozi wa CCM wakimlaki Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa katika Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto alipopita kutia baraka ofisi hizo akielekea kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili ya kumpongeza.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akitia saini kitabu cha wageni cha Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto.
Waendesha boda boda wa Gongo la Mboto wakitia mbwembwe katika mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Msafara wa Jerry Silaa ukiwasili uwanjani hapo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Gongo la Mboto.
Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akipunga mkono kwa wananchi, WanaCCM waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza kuchaguliwa nafasi nyeti ya Chama cha Mapinduzi.
Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM taifa Jerry Silaa akivishwa skafu ya chama mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Gongo la Mboto.
Jerry Silaa akivishwa lubega ya kimasai baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana Gongo la Mboto jijini Dar.
Pichani juu na chini ni Baadhi WanaCCM wa kata ya Gongo la Mboto wakimpongeza Jerry Silaa baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM Taifa wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza katika viwanja vya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Gongo la Mboto wakubwa kwa wadogo waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Wanenguaji wa Mashujaa Band wakicheza staili ya Boda boda na Wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara.
"UTU UZIMA DAWA KWA RAHA ZETU"...Rappa wa Bendi ya Mashujaa akicheza sambamba na kinamama wa Kata ya Gongo la Mboto wakati wa sherehe za kumpongeza Jerry Silaa zilizoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
Jukwaa kuu la viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki Gongo la Mboto jijini Dar.
Katibu Mwenezi wa CCM Mtwara Bw. Haroun Maarifa akitoa salamu kwa wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Wana CCM wa Gongo la Mboto wakitia manjonjo kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Ukonga Mh. Eugene Mwaiposi akizungumza na wananchi wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo ya Wakazi wa jimbo lake yanayopangwa kufanywa na Serikali kwa manufaa ya wakazi wa maeneo hayo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa akizungumza machache na wananchi wa kata ya Gongo la Mboto kabla ya kumkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhutubia wananchi katika mkutano huo.
Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa Jerry Silaa akisindikizwa Jukwaani kwa staili ya aina yake ya kufagiliwa njia na WanaCCM waliokuwa wakibiringika mpaka kwenye ngazi za jukwaa. Anayemsindikiza ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi.
"Karibuni kwenye Chama chenye mshikamano na Sera za Ukweli" ndiyo maneno ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa wakati akigawa kadi kwa Wanachama wapya wa Gongo la Mboto walipoamua kujiunga baada ya kukolewa na sera za CCM wakati wa mkutano huo.
Zoezi la ugawaji kadi kwa wanachama wapya likiendelea. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa.
Pichani juu na chini ni Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mbele ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa na viongozi mbalimbali wa Chama wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Mh. Jerry Silaa akizungumza na wananchi wa Kata yake ya Gongo la Mboto ambapo amewasihi viongozi wa CCM ngazi za Chini kuhakikisha wanafuatilia na kutafutia ufumbuzi kero zinazo wakabili watu wanaowazunguka.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi na wana CCM kwa ujumla kufuatia kuteuliwa na Mh.rais kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na kusema ofisi za chama zinatakiwa kuwa wazi kuanzia ngazi ya kata mpaka mkoa ili wananchi waweze kufika kutoa kero zao.
Aidha amewataka viongozi wenzake kufanyakazi kwa ushirikiano na uadilifu, na kuwa wale viongozi wachache wasio waadilifu watashughulikiwa kikamilifu ili kuleta ufanisi ndani ya chama.
Baadhi ya wananchi wa Gongo la Mboto wakichukua taswira ya Diwani wao Jerry Silaa wakati wa mkutano wa hadhara.
Mmoja wachekeshaji katika mikutano ya CCM wanaofahamika kama Aki na Ukwa akimwombea Dua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kuzungumza na wana CCM wa Gongo la Mboto.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na wananchi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na mmoja wa watoto waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
"Asante kwa kuonyesha upendo...Mume wa mtu mie" ndivyo anavyoonekana kusema Mh. Jerry Silaa akimwambia mwana CCM mkereketwa aliyekwenda kumfuta jasho kwa kutumia Khanga yake.

TAARIFA YA MSIBA WA GRACE CHAO

$
0
0

FAMILIA  ya Marehemu Mathew Ndesamburo Chao wa Mazimbu Morogoro, inasikitika kuwatangazia Msiba wa Binti yao Mpendwa Grace Chao kilichotokea leo asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

Mipango ya Mazishi kwa sasa inafanyika nyumbani kwa dada wa Marehemu Yombo kwa Abiola jijini Dar es Salaam na Maiti itasafirishwa kesho Jumaane kwenda Mazimbu Morogoro na kutolewa heshima kwa ndugu jamaa na marafiki waishio Morogoro Mjini na Mzumbe.

Jumatano Mwili wa Mpendwa wetu Grace Chao, utasafirishwa kutoka Mazimbu Morogoro kwenda Marangu Mamba kwa Makundi kwa mazishi.

Mwana Mzumbe na Morogoro kwa Ujumla tunaombwa sana kushirikiana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha Maombolezo.

Taarifa hii ni kwa Mujibu wa Kaka wa Marehemu, Edwin Chao.
            
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.

Neno La Leo: Ya Padri Mushi Na Ugumu Usiokuwepo Wa Kurudi Misri!

$
0
0
 Ndugu zangu,
Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.

Bado, kama taifa, tuko kwenye mshtuko wa kuawa kwa Padri Mushi kule Unguja. Swali bado linaning'inia vichwani; KWANINI?

Watanzania kwa asili ni ndugu, haya ya tofauti za kidini hayajawahi kuwa tatizo kwetu. Mathalan, asubuhi hii nilikuwa naongea na ndugu yangu kijijini Mahango, Madibira, Mbeya. Anaitwa Salim Mjengwa, yeye ni Muislamu, baba yake, Raphael Mjengwa ni Mkristo. Na kwenye familia yao wamechanganyika Waislamu na Wakristo. Kamwe haijawa tatizo kwao wala kwa sisi ndugu zao.

Jana jioni niliongea na Padri Manfred Mjengwa, naye ni mdogo wangu. Alikuwa njiani kwenda msibani Unguja kumzika Padri mwenzake na rafiki yake waliofanya kazi pamoja alipokuwa Zanzibar. Ni Padri Mushi. Ukristo wa Manfred sijapata kuuona ni tatizo kwenye ukoo wetu uliochanganyika kiimani. Hata mmoja wa watoto wangu nimempa jina la baba yake mdogo, anaitwa Manfred.

Ndugu zangu,

Kuna tulikotoka na tumeanza kupasahau. Nimepata kuandika yafuatayo, kuwa ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri. Hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna Wana wa Israel wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri.

Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.

Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.

Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ‘ Wao Wakristo’ na ‘ Sisi Waislamu’. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ‘ Nchi Yetu’ na maslahi yake.

Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.

Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).

Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.

Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.

Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.

Kuna hata wenye kufikia kutamka; ‘Nchi hii ina wenyewe’. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.

Ukiuliza utajibiwa; “Ah! Nchi ina wenyewe!”. Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.

Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.

Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya ‘kila mtu na lwake’. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.

Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.

Na hilo ni Neno la Leo.
Maggid Mjengwa,

Iringa,

0788 111 765, 0754 678 252

http://mjengwablog.co.tz/

WENGI WAMUAGA MAREHEMU GRACE CHAO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Ilikuwa ni majonzi sana katika tukio hili, kwa Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.

 Wafanyakazi wa CRDB Bank waliita kutoa heshima kwa Mwili wa Mfanyakazi mwenzao.
 Vijana wa Mzumbe Wengi sana walijitokeza kumuaga Grace katika safari yake hiyo ya Mwisho.
Marafiki na vijana wa Mzumbe wakimfariji kaka wa Marehemu Edwin Ndesamburo Chao (kulia) kufuatia msiba wa dada yake.

Skylight Band yatoa shukrani kwa mashabiki na kutambulisha nyimbo mpya ya “Nasaka Dhoughs”.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Bendi ya Skylight Anneth Kushaba akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo ambapo ametoa shukurani kwa mashabiki na waandishi wa habari kwa kuiunga mkono bendi hiyo pamoja na kuwa bado ni changa. Ameongeza kuwa bendi hiyo inapiga muziki aina ya ‘Afro Pop’ kutokana na falsafa yao ya muziki na mahitaji ya soko la muziki wa ‘Live’ hapa Tanzania. Kulia ni mwanamuziki Joniko Flower.
Kushaba amewataka mashabiki wa muziki kuhudhuria kwa wingi katika show yao watakayopiga katika kiwanja chao cha nyumbani cha Thai Village kuanzia saa tatu usiku.
Mwanamuziki Joniko Flower wa Skylight Band akitoa kionjo kwa waandishi wa habari waliohudhuria hafla fupi ya kutambulisha nyimbo mpya na kuwashukuru mashabiki wao kwa kuwaunga mkono.
Aneth Kushaba AK 47 akiongoza kundi la vijana wa Skylight Band kutoa burudani wakati wakitambulisha nyimbo yao mpya ya "Nasaka Dhoughs" iliyomo kwenye albam yao yenye nyimbo nane inayokaribia kutoka hivi karibuni.
Sam Mapenzi akijimwaga na sebene la Carolina.
Mwanamuziki Sony Masamba akikamua.
Salma Yusuf uzao wa BSS akionyesha kipaji chake kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa single mpya ya Skylight Band.
Na Mo Blog.
Kwa niaba ya bendi nzima ya Skylight Mkurugenzi Mkuu Anneth Kushaba ameomba ushirikiano kutoka kwa mashabiki, hamasa na kuungwa mkono katika kuendeleza burudani na kuleta ladha mpya ndani ya fani ya Muziki.
Pia ameomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuendeleza juhudi za kuwahakikishia wapenzi wanaohudhuria maonyesho yao Thai Village kila Ijumaa wanapata muziki wenye kiwango bora kama unasikiliza CD.
Kushaba amesema wamefanikiwa kuboresha sauti kwa kuongeza aina ya vyombo vinavyotumika katika maonyesho ya kimataifa.

Peter Amandus ashinda Tshs 5,000,000 za DStv Rewards

$
0
0
Peter Amandus mfanyakazi wa TRA (kati) akifurahia Tshs 5,000,000 alipozawadiwa na DStv kwa kulipia akaunti yake ya DStv kabla ya kukatika. Kulia ni Barbara Kambogi (Meneja Uhusiano), Ronald Shelukindo (Meneja Uendeshaji) na Furaha Samalu (Meneja Masoko) wa kampuni ya MultiChoice Tanzania.
 

WITO KWA MABLOGA WETU KUWA WABUNIFU BADALA YA KUIBA AU KUNUKUU TU KAZI NA PICHA ZA WENZAO BILA IDHINI

$
0
0
Ukingoni mwa Ziwa Nyasa- Revo Meza 
Ukingoni mwa Ziwa Tanganyika- picha ya Revocatus Meza, Desemba 2012. Wimbi la “blogging” liliikumba dunia kati ya 1995 hadi 1998 na kuanza kumea kwetu Tanzania kupitia mwanahabari Ndesanjo Macha miaka kumi iliyopita. Wakati Ndesanjo anaanza kublogu si wengi tuliomwelewa. Nakumbuka alivyokua akiniongelea juu ya fani hii kwa hamasa kwenye 2002. Baadaye kidogo aliendesha Jikomboe, blogu lililokua na taswira ya majani mabichi ya ukoka. Enzi hizo hakukua na hata senti moja aliyoichuma. Ndesanjo Macha 
Ndesanjo Macha- mwasisi wa blogu Tanzania Ndesanjo alikua akisema blogu ni dunia ya kesho ya mawasiliano. Wakati huo vyombo vikubwa vya habari nchi zilizoendelea vilianza kuona umuhimu wa blogu vikaanza kuunda idara pembezoni mwa tovuti zake mama. Kwetu wenye magazeti wengi hawakupenda wanablogu;waliwaona washindani. Mwaka ambapo wanablogu wetu walianza kuchomoza ilikua 2006 baada ya kifo cha wapenzi wawili wa Kitanzania waliouliwa kinyama Marekani. Blogu la Michuzi (ambalo halikua maarufu kama leo) na Radio Butiama (inayojulikana kwa jina Podcast) zilisimama dede kutangaza habari hizo. Hapo ndipo miye binafsi nilipoanza kuona namna wanablogu walivyokuwa na mwendo mkali - zaidi ya vyombo vya habari vya kijadi. Niliingia rasmi uwanjani mwaka 2007- nikisaidiwa na Ndesanjo na wanabloga wengine walionitangulia; akina Simon Kitururu, Jeff Msangi (Bongo Celebrity) mathalan. Nilichogundua siku za mwanzo ni kwamba Blogaz husaidiana sana. “Ukiwa mbinafsi huendelei kama Bloga” alisisitiza Ndesanjo. Goats feeding on rubbish 
Mbuzi wetu Bongo wakila kila aina ya takataka mitaani. Nyama yake tamu. Lakini je, ina nini kinachotudhuru tusichokijua? Nilipiga picha hii, Zanzibar, mwaka 2011. Leo Jikomboe na ule ukoka havipo tena. Ndesanjo, mwasisi wa blog za Kiswahili duniani, anafanya kazi shirika la habari- Global Voices. Kati ya mamia ya waandishi wa shirika hilo la kimataifa, Mtanzania huyu anaongoza kwa habari asilia za uchambuzi zaidi ya 4,200 . Tofauti ya mtu kama Ndesanjo na baadhi ya blogaz ni kwamba yeye kiasilia ni mwanahabari hivyo anachanganya ujuzi na mitindo hii miwili ya kusanifu matukio. Si ajabu mwaka jana Ndesanjo alishinda tuzo la Mwanablog bora wa Afrika.
Lugha ya blogaz na vyombo asilia vya habari zi tofauti. Wanahabari lakini ni watu waliosemea sawasawa kazi zao na kufuata utaratibu wa lugha, kusahihisha na kuhariri kazi. Bloga ni mtu yeyote tu mitaani au kijijini anayetaka kuelezea jambo. Kuhe -samaki- by Revo Meza 
Samaki aitwaye Kuhe katika Ziwa Tanganyika. Picha nimeletewa na mwandishi Revocatus Meza. Mvua ya blogaz Tanzania imejaza bahari safi tena ya faraja. Blogaz ni wengi tena wa kila rangi na jinsia; wanatupasha matukio kila sekunde! Wakati tukianza, wanawake hawakua wengi. Mwaka jana mshindi wa Blogaz bora Bongo alikuwa Mwanamke na Nyumba. Nyingine zimekuwa makutano au baraza la maoni na malumbano muhimu- mfano Jamii Forums, iliyoundwa 2006. Zipo zenye mafunzo mazito- angalia Al Hidaaya inayofunza masuala ya Kiislamu na Korani tutaelewana n’na maana gani. Zile zenye kurasa moja (kama zangu) zimegeuzwa viwanda vidogo; mathalan ya Maggid Mjengwa ambayo ni kijigazeti cha ajira. Ajira zinazowahudumia na kuwafariji wanahabari wake. Mara nyingine zina maudhi maana hata kuzifungua zinakua shida maana matangazo yamejazana pale juu kiasi ambacho si tena habari bali duka. Ama kweli mtandao umekuwa biashara. Uzuri upo ndiyo; ubaya tuuseme pia!Msukuma Mkokoteni-Magomeni 2009-pic by F Macha 
Msukuma mikokoteni akitotwa jasho saa za alasiri, mitaa ya Magomeni Mapipa. Niliipiga picha hii mwaka 2009, Dar es Salaam. Watanzania tunakwenda na wakati si uongo. Maana ukitazama wenzetu nchi zilizoendelea wanaelekeza kila jicho katika mtandao na inteneti. Maduka makubwa makubwa asilia nchi magharibi yanapata hasara na kufunga virago vyake. Mwishoni mwa mwaka jana asilimia 25 ya biashara zote nchi zilizoendelea zilitokana na makampuni yenye mauzo ya mitandaoni – yakaingiza dola bilioni 1.7! Linaloongoza sasa hivi ni Amazon inayouza kila kitu bei rahisi na kwa ufanisi zaidi kuliko maduka asilia. Makisio ya faida ya Amazon mwaka jana yalikuwa dola bilioni 63. Uingereza duka maarufu la muziki, sinema na vitabu- HMV- lilipunguza wafanyakazi mwezi jana na tetesi ni kuwa wameshafifia kibiashara. Ama kweli mtandao ndiyo soko mzazi wa biashara leo na kesho (kama alivyosema Ndesanjo) na wanabloga wetu wanakwenda na wakati. Mwandishi gwiji wa Kiswahili Ebrahim Hussenaliwahi kuandika “wakati ukuta ukipigana nao utaumia.” Ndiyo maana wafanya biashara wanatangaza bidhaa kupitia blogu. Ndiyo hali halisi ilivyo. [caption id="attachment_1655" align="aligncenter" width="500"]Kitabu kipya cha Prof Said Ahmed 
Kitabu kipya cha Prof Said Ahmed[/caption] Kitabu kipya cha Mwandishi nguli, Profesa Said Ahmed- Mhanga Nafsi Yangu- ambacho kinamwangalia mwanamke wa Kibongo anayekwenda kusoma ughaibuni. Kimetolewa na Sasa Sema (Longhorn) wa Kenya,2012. Ila tutathmini zaidi hilo... Blogu zilibuniwa kutangaza mambo na kadhia ambazo hazipo ndani ya vyombo habari mama na runinga. Zilibuniwa kumfaidisha mwananchi yeyote wa kawaida akibeba kamera na simu yake mkononi akaeleza habari za pale anapoishi. Hicho ndicho chanzo... Kama hukua na nafasi kuna Twitter ambayo ni fupi zaidi (maneno 30 tu!). Zana hizi ni muhimu sana kwa jamii ya leo. Hizi ni “habari za raia wa kawaida” . Umuhimu wa Blog, Twitter na You Tube umeonekana pale yalipotokea machafuko na harakati mbalimbali duniani kama Tunisia, Misri, Libya na Mashariki ya Kati nzima miaka miwili iliyopita. Dhoruba za mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi zilisambaa dunia nzima haraka kutokana na uwezo huu muadhama. Nguzo zake ndizo hizo. Google ambaye hulipa matangazo ya biashara kutokana na “maudhui ya habari” husisitiza wanablogu na waandishi kuwa wa kweli na kutochezea kazi za wenzao. Kwetu Bongo hapana. Miaka ya karibuni makampuni makubwa makubwa na mabenki kama National Microfinance (NMB) yanasaidia kuwekezea wajisiria mali wadogo wadogo (yaani Blogaz). Mara nyingi makampuni haya hayaangalii kama wanablog hawa wananukuu kazi za wenzao, wanaandika mambo yao wenyewe au wanakopi tu na kubandika. Logo- Sema Ndiyo-2 
Nembo ya kutetea haki za wanyama pori wanaouliwa ovyo. Kampeni hii inaongozwa na Kidon Mkuu Ngoille Mkuu, wa Arusha. Dili zinapatikana kwa kujuana juana, mathalan. Bahati mbaya kumezuka mtindo wa wanablogu wengi kutwaa kazi na picha za wenzao bila kuandika zimetoka wapi. Ukilinganisha sasa hivi Blogu zetu Tanzania ni tofauti sana na za nchi nyingine maana wengi hatuandiki vitu tulivyovibuni au tunavyoviona. Mmoja akishaandika tu basi wengine wote tunakopi na kubandika tu bila kuangalia sana kazi ikoje. Siku Google na mashirika miliki ya hizi blogu wakifahamu yatakua mengine. Kwa sasa tunajificha ficha tu. Saria akikochi vijana Dodoma 
Mwanamichezo na mwanahabari Israel Saria akiwa kazini na vijana Dodoma miaka ile ya Themanini. Niliongea na Israel Saria, anayeendesha blogu-tovuti la Michezo Tanzania (Tanzania Sports) tokea London karibuni. Saria ameendesha shughuli hii toka 2005 na anafadhiliwa na NMB. Mbali ya kuwa mtangazaji wa michezo BBC, Saria ni mwalimu rasmi wa mchezo wa mpira wa nyavu aliyekuwa kocha miaka mingi Tanzania. Alipendekeza wawekezaji kuangalia thamani ya blog mbalimbali kabla ya kuzipachikia matangazo: “Hebu linganisha blogu zetu na za majirani wa Kenya. Wakenya wengi huandika mambo wanayobuni. Sisi tunakosa ubunifu na uhalisia. Mwenzetu akiandika habari- baada ya dakika tano –mabloga wengine wote tunainukuu na kuitangaza ikiwa imejazana makosa. Tunalipua tu. Hatuna hata muda wa kuichunguza au kuihariri. Tunadhani kublogu ni suala la umaarufu na kuonekana kwamba na mimi nipo; eti sitaki nionekane kwamba nimekosa ile habari iliyotangazwa na mwenzangu!” Saria anaongeza kusema kwamba wengi wetu tunashindwa kutambua kwamba Google huwa wanajua na kuangalia kazi asilia. “Ukishatundika tu kazi yako, baada ya dakika chache tayari inasajiliwa kama ni mali yako. Yeyote anayeinukuu au kuitumia hatambuliwi kama mwenye hiyo kazi.” Mabloga wengi Bongo basi wanarudia rudia tu kazi za wenzao kwa kuzitapika na kuzitafuna kama ambavyo ng’ombe wanavyofanya baada ya kula majani. Matokeo baadhi ya blogu leo zimegeuka mabango ya matangazo badala ya kazi muhimu za kifasihi. Zipo blogu nyingi zinazobuni mambo- lakini pia zipo ambazo zinacheza tu. MaandaziPicha ya Maandazi toka tovuti la Taste of Tanzania. Picha ya Miriam Rose Kinunda... Miriam Rose Kinunda anayeendesha tovuti-blogu ya mapishi (Taste of Tanzania) amekuwa akisanifu blogu na kusaidia wenzake kuzijenga toka 2004. Anasema ni mara nyingi sana ambapo kazi na picha zake zimetumiwa bila idhini. “Awali nilikua nikiblogu Kiswahili na Kiingereza, lakini kutokana na huu wizi wa kazi, nimeondoa kabisa kitengo cha Kiswahili nikabakisha Kiingereza kwa wasomaji wa kimataifa.” Miriam ambaye karibuni atatoka na kitabu chake cha mapishi anataja mfano ambapo tovuti moja maarufu ya Kenya iliiba kazi na picha zake. Akaamua kuwapigia simu. “Baada tu ya dakika tano, jamaa walinitumia barua pepe kunitaka radhi. Walionyesha namna walivyo waungwana.” Miriam Rose Kitunda 
Miriam Rose Kinunda Je nini kifanyike? Saria na Bi Kinunda wanashauri wawekezaji (mathalan benki inayowafariji wanablogu kama NMB) kufadhili na kusaidia tu wale wanaokua wabunifu na wanaofuata kanuni za fani hii muhimu katika jamii. Kigoda 
Kigoda nyumbani kwa mpigania utamaduni wetu na mfanyabiashara mashuhuri wa Dar es Salaam, Mwafrika Merinyo anayeendesha shughuli za Afrika Sana. Nilipiga picha Novemba 2011.Makala hii iliandikwa pia kwa Kiingereza katika safu ya Mwandishi gazeti la Citizen mwezi jana

Mstahiki Meya Jerry Silaa akabidhi vyeti kwa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya St. Anthony jijini Dar.

$
0
0
Mgeni rasmi katika mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa shule hiyo kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hizo.
Padri akiendesha ibada wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akifuatilia ibada hiyo kubariki mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John na Mkuu wa shule hiyo Bro. Ismail Edward ( wa pili kulia).
Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya St. Anthony wakisikiliza mahaburi wakati wa ibada hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kwenye sala maalum wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakisoma sala za mtu mmoja kuombea mambo tofauti ikiwemo Amani kwa Taifa.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari St. Anthony wakimwogoza mgeni rasmi kwa madoido ya aina yake wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya shule ya Sekondari St. Anthony akiwa ameambatana na viongozi wa shule hiyo tayari kuanza rasmi sherehe za mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakishiriki kuimba wimbo wa shule.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano wakiimba wimbo wa kuwaaga dada zao na kaka zao mbele ya mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari St. Anthony wakifanya igizo la Dr. Livingstone lililowavunja mbavu wazazi na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa hoi kwa kucheka kutokana na igizo la Dr. Livingstone. Kushoto ni Makamu Mkuu wa pili wa Shule hiyo Rempta Adams akifuatiwa na Mkuu wa Shule hiyo Bro. Ismail Edward.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo amezungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunza, mabadiliko ya mara kwa mara ya Mitaala na matamko juu ya Elimu, tabia ya wanafunzi kuiga tamaduni za Ughaibuni na Ukosefu/kukatika kwa nishati ya Umeme.
Sehemu ya wazazi na walezi waliohudhuria mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akikabidhi taarifa ya shule yake kwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akisoma risala ya wanafunzi wa kidato cha sita mbele ya mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akimkabidhi mgeni rasmi risala hiyo.
Mwanfunzi Samwel Mwanzini akionyesha kipaji chake cha kuimba na kupiga kinanda ambapo alishangaza wengi kwa uwezo aliokuwa nao.
Mwanfunzi Tracy Raymond Ndanshau wa kidato cha tano PCM akiimba sambamba na Mwl. Nikiza Bwenge katika mahafali ya 20 ya kidato cha sita.
Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John (kulia) akisoma risala fupi ya kukabidhi wahitimu kidato cha sita 2013 kwa wazazi rasmi Bw. na Bibi Amos Bujiku wakati wa mahafali hayo.
Wazazi rasmi rasmi Bw. na Bibi Bujiku wakiwapokea rasmi wanafunzi Mary Bujiku na Edward Mugyabuso kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha sita kwenda kuwalea kiroho.
Mkuu wa Shule ya sekondari St. Anthony Bro. Ismail Edward akisoma risala kwenye mahafali ya 20 ya kidato cha sita ambapo amewasihi wanafunzi wanaohitimu waendelee kutunza kumbukumbu ya shule hiyo na kuwa mabalozi wazuri wa St. Anthony kwa kuwa wazalendo wa kweli waliotayari kulijenga na kulilinda taifa letu na kukabiliana na changamoto za dunia ya leo hususani gonjwa hatari la Ukimwi na matatizo mengine yanayoikumba Tanzania.
Meza kuu ipitia risala ya Mkuu wa shule hiyo.
Picha juu na chini Mgeni rasmi Mstahi Meya Jerry Silaa akizungumza wakati wa mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya St. Anthony ambapo ametoa pongezi kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo na kuongeza kuwa kwa sisi Watanzania Elimu ni nyenzo muhimu sana hasa katika mbio zetu za kupambana na maadui watatu; ujinga, maradhi na umaskini ambayo ni Silaha pekee ya kuwashinda maadui hao wote watatu.
Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita wakimsikiliza mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Wahitimu wa kidato cha sita wakielekea kukabidhi zawadi kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea zawadi hiyo.
Mgeni rasmi akifingua zawadi hiyo mbele ya wahitimu hao.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na wahitimu wa kidato cha sita ambapo walimtaka kuiweka ofisini kwake ili aendelee kuwakumbuka.
Picha Juu na Chini Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi vyeti na zawadi kwa wahitimu wa kidato cha sita wa St. Anthony katika sherehe za mahafali ya 20 shuleni hapo.

GLORIOUS WORSHIP TEAM KUADHIMISHA MIAKA 2 J'PILI HII ATRIUMS HOTEL

$
0
0
 
Mmoja wa kiongozi wa kundi la 'Glorious Worship Team akiongea jambo na Wandishi wa habari hawapo pichani
 
Kundi la 'Glorious Worship Team, wakiimba nyimbo
WASANII wa kundi la nyimbo za injili nchini 'Glorious Worship Team' keshokutwa Jumapili, Februari 24 mwaka huu wataadhimisha sherehe ya kutimiza miaka miwili ya kueneza injili ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya The Atrium, iliyopo Sinza Afrika Sana. Kiingilio katika hafla hiyo ni shilingi 5,000/= na wote mnakaribishwa.

mama salma kikwete aongoza hafla ya kuchangia wanawake matatizo ya afya,zaidi ya mil 142 zapatikana

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda akimpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda pichani kushoto akizungumza machache mbele ya meza kuu kabla ya kumpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal.

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Bwa.Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia $ 10,000 kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar.

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT),Bwa.Benno Ndulu cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia Milioni Kumi kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar.

Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal pichani kulia akizungumza machache,ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi Milioni mbili katika hafla hiyo.

Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na kumkabidhi cheti cha heshima Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshim mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfast kutoka Clouds FM,Said Bonge a.k.a Bonge Barabarani ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi laki tisa.

Makofi ya pongezi na shukurani kwa Bonge Barabarani yakipigwa.


Mama Salma Kikwete akimkabidhi mmoja wa Wakilishi wa Kampuni ya ndege ya Flight Link cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshima Meneja mahusiano wa PPF,Lulu Mengele ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo,kulia kwake akishuhudia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal..

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) mara baada ya kuifanikisha hafla hiyo kwa kiasi kikubwa.

Mmoja wa Waratibu wa hafla ya Montage Charity Ball,Barbra Hassan akiwakaribisha baadhi ya viongozi mbalimbali wa kiserikali,mabalozi na wageni waalikwa wengine waliofika kwenye hafla hiyo ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.

















Pichani juu ni wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete.

Kalunde Band wakitumbuiza jukwaani

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akipewa kampani na baadhi ya wanamuziki wenzake jukwaani,wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.

Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiongozwa na MKurugenzi wao Mtendani (wa tatu kulia),Steve Gannon wakiwa katika picha ya pamoja,aidha kampuni hiyo pamoja na kudhamini hafla hiyo pia ilichangia kiasi cha shilingi milioni tano



Baadhi ya magauni yakinadiwa kwa staili ya kipekee kabisa,kwa ajili ya kuchangia mfuko huo wa kuwasiadia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball.

PICHA ZOTE NA Michuzijr Blog.
Viewing all 4405 articles
Browse latest View live