Quantcast
Channel: MRISHO'S BLOG
Viewing all 4405 articles
Browse latest View live

Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro yashirikiana na Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front.

$
0
0
Picha juu na chini ni Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza mazingira.
Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro imeamua kuialika kampuni ya usafi ya Green Waste Pro baada ya kuona juhudi zao za kuweka Manispaa ya Ilala safi na mabadiliko yanaonekana ndipo wakaamua kushirikiana nao katika zoezi la kusafisha fukwe hizo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo iliyojipangia kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza mazingira.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena (kushoto) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Kivukoni Front baada ya kupata mwaliko kutoka Hoteli ya Hyatt Regency wa kushiriki katika kusafisha fukwe hizo.
Mwananchi asiyefahamika akiwa amechapa usingizi huku akiwa amejifunika gunia chafu na kulifanya kuwa shuka katika kichaka cha fukwe za Kivukoni Front wakati zoezi la usafi likiendelea.WADAU huyu jamaa hatuna uhakika kama naye ni sehemu ya uchafu au ndio nyumbani?? Tembea uone.
Picha juu na chini ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro wakiwa wamebeba mafurushi ya lundo la uchafu uliokusanywa kutoka kwenye fukwe za Kivukoni Front zilizopo karibu na Hoteli hiyo.
Moja ya magari ya kukusanya uchafu ya kampuni ya Green Waste Pro likiwa limesheheni lundo la uchafu uliokusanywa toka kwenye Fukwe za Kivukoni Front baada ya kusafishwa na Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa kushirikiana na kampuni ya usafi ya Green Waste Pro.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd wakibadilishana mawazo baada ya kuhitimisha zoezi la kusafisha fukwe za Kivukoni Front na kuishukuru kampuni ya Green Waste Pro kwa kuitikia wito.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Hyatt Regency na kampuni ya Green Waste Pro baada ya zoezi la usafi.

NHIF YADONDOSHA BONGE LA HAFLA KUWASHUKURU WANAHABARI KWA KUFANIKISHA KONGAMANO MKOANI MTWARA

$
0
0
12
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya kujipongezana na kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa Makonde mjini Mtwara,baada ya kumalizika kwa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika jana kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani humo.2 
Maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka kulia ni Grace Michael na Dr. Ahena Mramba Rose Gabriel wakiwa katika hafla hiyo.
4 
Mkurugenzi wa Tathmini na Uhai wa Mfuko na Takwimu NHIF , Bw. Michael Mhando akifurahia jambo na Grace Michael Ofisa Masoko wa mfuko huo wakati wa hafla hiyo kulia ni ni Angela Mziray
5
Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Mgaya Kingoba wa Habari Leo na wenzake7 
Steven Mhina kulia akiwa na Angel Akilimali kushoto wote kutoka Radio Uhuru
8 
Wanahabari mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika hafla hiyo
10 
Ofisa wa Masoko wa NHIF Grace Michael wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari
11 
Kutoka kulia ni Catherin Sungura kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Grace Michael na Faraja Kihongole kutoka Chaenl Ten
14 
Hawa jamaa walikonga nyoyo za wanahabari kwa vichekesho vyao.
15 
Gladness Mboma wa pili kutoka kulia na wanahabari wenzake wakiwa kaatika hafla hiyo.
17 
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Moshi Chang'a akishukuru baada ya kupokea cheti chake kutokana na mchango wake wa NHIF katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba na kushoto ni Salome Manyama meneja wa tawi la NHIF makao makuu
16
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Moshi Chang'a akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba na kushoto ni Salome Manyama meneja wa tawi la NHIF makao makuu18 
Hapa ikiwa ni burudani kwa kwenda mbele
20 
Wanahabari wakacheza kwaito kama wanavyoonekana.
21 
Mchora Katuni King Kinya akitoa burudani jukwaani huku mpiga gitaa Yahya Mkango aliyewahi kufanya kazi na bendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam.

Kuhusu Wimbo wa MwanaFA uliokuwa utoke leo

$
0
0
                                                             TAARIFA KWA WADAU
Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) ungeanza kuuzwa kupitia njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za mkononi.

Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.
 
Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.

Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara.
Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu,pia kuboresha zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani hii itawafikia washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA, Kilimanjaro Band(Wana Njenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi wa kusubiri na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama  Zamani kama ilivyopangwa hapo awali.

Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa mnasubiri kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi kipya na moja ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40 katika tasnia ya muziki Tanzania umewaandalia.

Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc. unaomba uvumilivu na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki. Tunaamini kwamba subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.
 
Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.



Henry Mdimu

TALISS Swim Club yaitaka Serikali kuamka na kujenga Mabwawa ya kuogelea ya Umma yenye viwango.

$
0
0
Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed (mwenye miwani nyeusi) akizungumza na washiriki pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea yaliyoshirikisha Club mbalimbali na kwa rika tofauti yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors wauzaji wa magari ya kisasa hapa nchini yaliyofanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
Amesema Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha vilabu na watu binafsi wenye ujuzi wa kuogelea unaofikia kiwango cha kushiriki mashindano.
Aidha Bi. Najat Ahmed ameomba wadau zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kuiomba Serikali ijitokeze na kujenga mabwawa yanayohitajika kwa ajili ya watu kujifunza kuogelea ili kuweza kujiokoa katika ajali za majini.
Pichani juu na chini washiriki wa club mbalimbali za kuogelea wakipita mbele wazazi na makocha kwa ajili ya utambulisho.
Official wakijipanga tayari kuanza mashindano hayo yaliyohusisha Clubs mbalimbali kutoka sehemu tofauti.
Pichani juu na chini ni washiriki wajitosa kwenye bwawa hilo kuchuana katika mashindano ya kuogelea yaliyoratibiwa na TALISS Swim Club na kudhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar.
Picha juu na chini Sehemu ya watazamaji wakishuhudia mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
Picha juu na chini Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiwavalisha medali washindi wa mashindano hayo katika kategori mbalimbali. CFAO Motors imeamua kudhamini mashindano hayo baada ya kuona umuhimu wa vijana kujua kuogelea ili kuweza kujiokoa katika majanga yanayohusiha ajali za majini zinazopelekea vifo vya watoto ikiwa ndio lengo la TALISS.
Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed akikabidhi medali kwa mmoja wa washindi wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne Mcintosh ambaye pia alikuwa MC katika mashindano hayo akikabidhi vikombe kwa washindi wa jumla walioshiriki TALISS Swimming Championships 2013.
Umati wa watu wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa pamoja makocha waliohudhuria kushuhudia mashindano ya kuogelea ya TALISS yaliyohusisha vilabu kutoka sehemu mbalimbali.
Pichani juu na chini baadhi ya wageni waliohudhuria kutazama mashindano ya kuogelea katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) wakikagua gari mpya aina ya Nissan Y62 inayosambazwa na Kampuni ya CFAO Motors.

KHADIJA KOPA, ISHA MASHAUZI WATOANA KIJASHO DAR LIVE

$
0
0
 
Malkia wa mipasho, Khadija Kopa, akionesha umahiri wake wa kutikisa nyonga.
 
Mashabiki wanaomfagilia Isha Mashauzi wakiwa wamevamia steji baada ya kuwadatisha.
 
Aziza Abul ‘Bonge’ wa TOT Taarab akikamua.
 
Malkia wa mipasho akiserebuka na mmoja wa mashabiki wake aliyepanda jukwaani kumtunza.
 
Wakali Dancers wakiwajibika jukwaani.
 
Shabiki akimtunza Malkia wa mipasho baada ya kukunwa na mipasho.
 
Isha Mashauzi akikamua.
 
Mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.
WAKALI wa miondoko ya muziki wa mwambao nchini, Malkia wa miondoko hiyo, Khadija Kopa akiwa na Kundi la TOT Taarab na Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ jana waliugeuza Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live kuwa uwanja wa mapambano baada ya kushindana kutoa burudani kwa kuonesha makali yao na kuwafanya mashabiki kila mmoja kumtaja mshindi wake.
Kabla ya wakali hao kuanza kuhenyeshana jukwaani burudani hizo zilianza kwa kunogeshwa na shoo kali ya washiriki wa shindano la Mic King linaloendeshwa ukumbini hapo kila Jumapili. Baada ya washiriki hao wanaowania gari, kundi la Wakali Dancers lilivamia jukwaa na kufanya vitu vyake pia.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )

Skylight Band yaendelea kutikisa kiwanja chao cha Nyumbani @ Thai Village Masaki jijini Dar.

$
0
0

Vijana wa SKYLIGHT BAND Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi wakiporomosha sebene kwa mashabiki wao kwenye Show ya aina yake ambapo walitambulisha nyimbo yao mpya kwa mashabiki wao inayofahamika kama "Nasaka Dough".
Mashabiki wakiburudika na SKYLIGHT BAND...Njoo na wewe Ijumaa hii uburudike pia.
Uzao wa BSS Salma Yusuf akipagawisha mashabiki wa SKYLIGHT BAND na mduara (mambo ya pwani). Pichani juu na chini wake kwa waume wakiwa wamefurika kwenye dancing floor kuonyesha umahiri wao katika mduara.
Kwa raha ya mduara mpaka wengine wanalala chini na kuzungusha nyonga.
Hapo sasa twende kazi.....Martin Kadinda mzee wa Single Button naye yumo.
Kijana kasusiwa ahangaike nalo.
Mbonie Masimba aksihow love na Blogger King Kif.
Joniko Flower, Salma Yusuf na Aneth Kushaba AK 47 wakiimba na kucheza Twist.....Chezea Twist wewe ni Balaaa....
Mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakisakata Twist huku kijasho kikiwatiririka.
Utu uzima dawa tunajikumbushia enzi zetu....Wazazi wa Salma Yusufu wa SKYLIGHT BAND wakisakata muziki aina ya Twist uliokuwa ukiimbwa na Joniko Flower.
Mary Lukas akifanya yake kwa mashabiki wa SKYLIGHT BAND.
Mdau Eric Ndalu wakifanya nyao na Best Friend wake.

UN SG Message to the International Commission against the Death Penalty

$
0
0
UN Secretary-General's message to the International Commission against the Death Penalty
[delivered by Ms. Kyung-wha Kang, Deputy High Commissioner for Human Rights]
Geneva, Switzerland, 25 February 2013


I thank the International Commission against the Death Penalty for organizing this discussion, and I commend the critical role of civil society in mobilizing global support on this important issue.  The right to life is the most fundamental of all human rights.  It lies at the heart of international human rights law.  The taking of life is too absolute, too irreversible, for one human being to inflict on another, even when backed by legal process.  That is why the United Nations system has long advocated the abolition of the death penalty.  International and hybrid tribunals supported by the UN do not provide for capital punishment, nor does the International Criminal Court.

Since the General Assembly first voted on a moratorium in 2007, the trend against capital punishment has gained momentum.  In December 2012, the Assembly’s support for a moratorium was 111 in favour to 41 against, with 34 abstentions.  The resolution calls on States to progressively restrict the use of capital punishment and not to impose it for offences committed by persons below 18 years of age and pregnant women.  States were also asked to reduce the number of offences subject to the death penalty.

The sentiment towards abolition finds echoes in every region and across legal systems, traditions, customs and religious backgrounds.  Currently some 150 States have either abolished the death penalty or do not practice it.  I am therefore concerned that some countries with a longstanding de facto moratorium have recently resumed imposing the death penalty, and have even carried out executions.  Even well-functioning legal systems sentence and execute persons who have been ultimately proven innocent.  Wrongful convictions and miscarriages of justice have condemned innocent people to years of anguish on death row before being executed or exonerated.

In those States that continue to impose the death penalty, thousands of individuals are executed each year – often in violation of international standards, such as the right to fair trial and due process.  The death penalty is still used for a wide range of crimes, such as drug crimes, which do not meet the threshold of “most serious crimes”, and information concerning the application of the death penalty is often cloaked in secrecy.


Capital punishment is inconsistent with the mission of the United Nations to reaffirm faith in fundamental human rights and the dignity and worth of the human person.  A global moratorium is a crucial stepping stone towards full worldwide abolition.  I urge you to use this meeting to consider how to further this end.

I wish you a productive discussion.

BODI YA UTALII YASAINI MKATABA NA WAANDAAJI WA ONESHO LA UTALII LA INDABA

$
0
0
20
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga katikati wa tatu kutoka kulia, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki kushoto na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd wakisaini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha onesha la Utalii litakalojulikana kwa jina la Swahili Tourism Fair kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika nchini Tanzania kwenye ukumbi huohuo wa Mlimani City Dar es salaam kuanzia Oktoba 2-5 mwaka huu, Wanaoshuhudia tendo hilo la kusainiwa kwa mkataba huo nyuma ni Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na kulia ni Ian Kaduma Mwanasheria wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Kampuni ya Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd Pia ndiyo inayoandaa maonyesho makubwa ya utalii nchini Afrika Kusini yanayojulikana kama Indaba 21 
Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd akisaini mkataba huo huku Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akishuhudia tukio hilo kushoto ni Ian Kaduma Mwanasheria wa TTB
22
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd wakibadilishana mikataba mara baada ya kusainiwa katikati wanaoshuhudia ni Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki 23 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd wakionyesha mikataba mara baada ya kusainiwa katikati wanaoshuhudia ni Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki
1 
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB DK Aloyce Nzuki akijadili jambo na wakuu wake wa vitengo katikati ni Philip Chitaunga Meneja wa Huduma za Utalii na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Bi. Devotha Mdachi
2 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga akizungumza na Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki kabla ya kusainiwa kwa mkataba huo leo katikati ni Meneja Huduma za Utalii Philip Chitaunga na Mkurugenzi wa Masoko Devotha Mdachi
3 
Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd na Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd wakiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City tayari kwa kusaini makubaliano hayo wanaosalimiana na Ian Kaduma Mwanasheria wa TTB na Philip Chitaunga Meneja Huduma za Utalii TTB
4 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga akisalimiana na Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd mara baada ya kuwasili ukumbini hapo leo kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki na maafisa wa TTB
6
Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akiwatambulisha wakurugenzi wa ya kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga kulia ni Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd na kushoto ni Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd 7 
Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Utalii Bi Devotha Mdachi katikati akiwa katika picha ya pamoja na maafisa mbalimbali wa Bodi hiyo
8 
Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akiongozwa na Philip Chitaunga Meneja wa Huduma za Utalii Bodi ya Utalii TTB mara baada ya kuwasili ukumbini hapo leo
9 
Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko TTB Bi Devotha Mdachi kulia ni Geofrey Meena Meneja wa Masoko wa Bodi hiyo.
10 
Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akisalimiana na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii TTB Bw. Geofrey Meena mara baada ya kuwasili ukumbini hapo leo.
11 
Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akisalimiana na Mwanasheria wa Bodi ya Utalii TTB Bw. Ian Kaduma
12 
Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki
13 
Mkurugenzi wa Masoko TTB Bi Devotha Mdachi akizungumza katika hafla hiyo
14 
Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga, Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania , Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd na Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd wakisubiri kusainiwa kwa mkataba huo
15 
Maafisa mbalimbali wa Bodi ya Utalii, na Ubalozi wa Afrika Kusini wakishuhudia utiaji saini wa mkataba huo
17 
Maafisa kutoka Bodi ya Utalii na Wizara ya Fedha wakishuhudia tukio hilo.
18 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga akizungumza katika hafla hiyo
19 
Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania naye akatoa maneno yake ya hekima kwa kusainiwa mkataba huo.
24 
Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga, Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania , Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd na Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd wakiwa katika picha ya pamoja
25 
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba wa kuanzishwa kwa onesho la Swahili Tourism Fair
26 
Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga, Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania , Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd na Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa bodi ya utalii

MeTL GROUP yapokea tuzo ya ubora na thamani ya nembo ikiwa ni ishara ya kukubalika

$
0
0
Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya tuzo za ubora na thamani ya nembo kwa makampuni bora 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Raha Aashiq Sharrif (Kulia) akiwa Mwakilishi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Raha Preetkamal Bansal ( wa pili kulia) wakati wa hafla fupi ya Superbrands kukabidhi vyeti kwa makampuni bora kwa mwaka 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville ( wa pili kulia) aliyembatana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP Bi. Joyce Luhanga ( wa tatu kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo iliyoendeshwa na Taasisi ya Superbrands.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Na.Mo Blog Team
Taasisi huru ya Superbrands ambayo ni kubwa kuliko zote duniani, inayoratibu ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji, leo imekabidhi vyeti vinavyotambuliwa kimataifa vya utambuzi wa ubora wa bidhaa kwa kampuni zilizofanya vizuri nchini Tanzania kwa mwaka 2013/2014.
Tuzo za Superbrands ni miongoni mwa tuzo zenye thamani kubwa na zinazoleta heshima ya pekee ndani ya kampuni.
Hii ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kutolewa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake yapata miaka mine iliyopita.
Uamuzi na hatimaye utoaji wa tuzo husika unatoka baraza huru la wataalamu waliobobea katika masuala ya biashara, lakini lengo hasa likiwa ni ni kustawisha na kuhamasisha ari katika utoaji huduma zinazo zingatia ubora.
MeTL imekuwa moja wapo kati ya Makampuni yaliyopokea vyeti vya tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya tatu hapa nchini.

London fashion Week 2013

Neno La Leo: Ningependa Nikumbukwe Pia Kwa Mchango Wangu Huu Mdogo Kwa Nchi Yangu...!

$
0
0
Ndugu zangu,
Kama mwanadamu, wakati mwingine tujiulize; Je, ni yepi ambayo tungependa wanadamu wenzetu waje kutukumbuka nayo? Ni  yale ambayo tutayaacha nyuma yetu- legacy.

Leo niliposoma gazeti la Mwananchi nimekutana na tangazo hilo pichani. Inahusu  wito kwa wanafunzi kujiunga na kozi ya Diploma ya Elimu ya Watu Wazima na Endelevu kwa njia ya masafa.

Hilo ni wazo langu la tangu mwaka 2005. Ni wazo nililoliibua nikiwa na Bw. Edward Lugakingira pale kwenye mhagawa wa Hasty taste, Iringa.

Edward Lugakingira alikuwa Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima pale Iringa. Tulifahamiana kupitia makala zangu za kwenye Rai enzi hizo.  Kwa sasa Edward Lugakingira ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kwenye Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Makao Makuu, Dar.

Wazo lilianzaje?

Nilipoajiriwa na Shirika la Forum Syd nikitokea Sweden mwaka 2004 nilipangiwa kufanya kazi Iringa. Huko niliratibu pia mafunzo ya wakufunzi wa Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi.  Zaidi ilikuwa ni kozi fupi fupi za masuala ya mbinu za ufundishaji. Kozi haikuzidi siku 5. Nilizunguka mikoa kadhaa na kukutana na walimu hao.

Ni baada ya mwaka mmoja,  na baada ya kuwa na nafasi ya kuzungumza na wakufunzi wenyewe, ndipo liliponijia wazo la kuwa na kozi ndefu ya Cheti na Diploma kwa njia ya masafa. Kozi ambayo ingetoa fursa pia kwa washiriki kukutana na walimu wao kwenye - face-to-face kila baada ya muda fulani.

Na hakuna jambo ambalo mwanadamu unaweza kulikamilisha peke yako. Tangu mwanzo wa wazo, nilianza kwa kumshirikisha Bw. Lugakingira ambaye baadae, kwa bahati njema, alihamishiwa Makao Makuu ya TEWW. Hapo kasi ya mchakato wa kulifanikisha wazo kuu ikaongezeka.

Wadau zaidi wakajiunga katika harakati za kulikamilisha wazo kuu. Ni pamoja na Chama Cha Walimu Tanzania na Chuo Kikuu cha Linkoping cha nchini Sweden. Ubalozi wa Sweden nao ukaunga mkono jitihada zetu.

Hatimaye, miaka miwili iliyopita, Balozi wa Sweden , Bw, Lennart Hjalmaker alizindua rasmi mafunzo ya kozi hiyo kwa majaribio kwa kundi la wakufunzi 45 kutoka Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi.

Majaribio hayo yamekwenda vema kuliko ilivyotarajiwa. Na kwenye Bunge la Bajeti la mwaka jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Mh. Shukuru Kawambwa, alitangaza rasmi Bungeni , mpango wa Wizara yake kupanua programu hiyo kwa kusajili washiriki wengi zaidi. Tangazo hilo hapo juu ni matokeo ya mpango huo.

Naamini kwa dhati, kuwa aina hii ya programu za mafunzo kwa njia za masafa kwa watumishi walio kazini na wasio watumishi, itasaidia kuwajengea uwezo watumishi hao, na  hivyo, kuinua ubora wa kazi zao. Itainua kipato chao pia.

Kubwa zaidi, walengwa ambao ni  wananchi walio wengi, watafaidika, mathalan, kwa watoto wao na wao wenyewe, kama watu wazima kupata maarifa zaidi na yenye ubora. Hivyo, tija kwa taifa zima.

Hata kama si mkubwa sana, hakika, ningependa nikumbukwe kwa mchango wangu huu kwa nchi yangu.

Na naamini pia, ni wajibu wetu kuifanya kazi hii kwa pamoja. Na kuwa,  kazi ya kuyafanikisha haya yote ni yetu sote.  Ni kwa maendeleo ya nchi yetu, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi na kiimani. Ni kwa maslahi ya taifa letu.
Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro.
0788 111 768
http://mjengwablog.co.tz

SHINDANO LA MIC KING LAZIDI KUCHANJA MBUGA

$
0
0
Mshiriki Ally Zuberi akichana mistari.
Arnold Mathias akichana mistari kivyake.
Bahati Charles akiwaonyesha majaji kipaji chake.
Boniface Mirumbe akilishambulia jukwaa.
Cosmas Milanzi akiwa ‘amejaa kujiamini’.
Washiriki shindano la Miss Utalii Taifa wakifuatilia The King Mic kwa makini.
Majaji Abdallah Mrisho (kushoto) na Ali Baucha wakiwa makini kufuatilia shindano hilo.
Mhudumu wa Dar Live akifuatilia shindano hilo kwa utulivu.
Baadhi ya warembo wa Miss Utalii wakiserebuka.
Pozi la warembo wa Miss Utalii.
SHINDANO la The Mic King limezidi kupamba moto ndani ya ukumbi wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem, jijini Dar es Salaam, jana Jumapili ambako washiriki 11 walitoana jasho katika kuonyesha umahiri wa kuchana mistari ya hip hop.
Shindano hilo lilihudhuriwa na warembo watakaoshiriki shindano la Miss Utalii Taifa ambao wanafanya mazoezi ndani ya ukumbi huo. (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

Ads by Browse to Save Mon, Mar 4, 2013 at 12:16 PM 12:16 PM Message starred FROM zainul mzige TO recipients Skylight Band yazidi kuwapa raha mashabiki wake kwenye kiwanja chao cha nyumban

$
0
0
Kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi Kikosi kazi cha SKYLIGHT BAND kikimwaga sebene kwa mashabiki wao Ijumaa ya mwisho wa wiki kwenye kiota chao cha nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar.
Wazungu wakionekana kupagawa na Bolingo lililokuwa likiporomoshwa na vijana wa Skylight Band kwenye Uwanja wao wa nyumbani Thai Village.
Sam Mapenzi wa Skylight Band akitunzwa na shabiki wake.
Mdau akishow love mbele ya Camera yetu.
Warembo walikuja kusheherekea Birthday ya rafiki yao Barbara.
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani sambamba na Mary Lukas wakilisongesha.
Mashabiki waliacha kucheza na kuanza kuangalia vibwanga vya wanamuziki wa Skylight Band.
Kutoka kushoto ni Salma Yusuf, Aneth Kushaba AK47 na Mary Lukas wakionyesha manjonjo yao kwa mashabiki.
Birthday Girl Barbara akisakata rhumba na marafiki zake.
Aneth Kushaba AK47 akiwajibika jukwaani.
Mary Lukas wa Skylight Band akimwimbia shabiki wake aliyetokea kupagawa na uimbaji wa binti huyo akiwa haamini macho yake.
Mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kuburudika na muziki mzuri kutoka kwa vijana wenye vipaji.
Mkali wa Hip Hop nchini Fareed Kubanda a.k.a FID Q akishow love na Blogger King Kif. Fid Q ni mara yake ya kwanza kufika kushuhudia show ya Live ya Skylight Band na aliwapa big up sana vijana kwa kazi nzuri.

KILI MARATHON

$
0
0
 
Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi
 Wanariadha kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.



Wakenya walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza  katika mbio hizo za mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph alebeba Medali ya Dhahabu.



Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.

DStv REWARDS YAENDELEA KUIBUA MAMILIONEA: AHMED SALIM SALEH ASHINDA Tshs.5,000,000

$
0
0
Ahmed Salim Saleh, mshindi wa Tshs, 5,000,000 za DStv Rewards akiwa na uso wa furaha huku ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa.
Katika muendelezo wa kampeni ya DStv Rewards kampuni ya MultiChoice Tanzania inayo furaha kumtangaza rasmi mshindi wake wa tatu. Mshindi huyo ni Ahmed Salim Saleh, mfanyakazi wa Access Bank ya jijini Dar-es-Salaam.

Malaika Event Rentals Showcase Their Gorgeous Set For Events

$
0
0
Malaika Team wakitoa maelezo kwa wateja waliofika kwenye maonyesho ya bidhaa wanazozikodisha kwa ajili ya matukio na hafla mbali mbali zikiwemo Harusi, mikutano, sherehe za kuzaliwa n.k
Baadhi ya wateja wakiangalia thamani hizo zenye ubora na za kupendeza.
Wow this is what i was looking for....!!!
They Rent Chiavari Gold & Silver and Folding Chairs, Tables and Table Linen for Small and Large Events. They can be used in weddings, Anniversaries, Dinner Parties, Birthdays and Corporate Events.
You can Contact them through +255 754 298 554, +255 789 333 888, and +255 754 474 709 Email: malaikadesings@gmail.com
 
Kazi za mikono za Malaika Rental and Design.
Baadhi wateja wakipata maelezo juu ya mipangalio na upambaji wa meza na viti kwa ajili ya matukio tofauti kutoka Malaika Team.
"This one is Amazing i Love the Colour Darling"....!

KAIMU BALOZI WA TANZANIA NCHINI UJERUMANI AKUTANA NA UJUMBE WA BODI YA UTALII

$
0
0
4 
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula kushoto akizungumza na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki wakati yeye na ujumbe wake walipomtembelea Mh. Balozi na kuzungumza naye mambo mbalimbali ukiwemo mkakati wa bodi hiyo katika kutangaza utalii wa Tanzania kupitia balozi zetu nchi mbalimbali za ulaya hasa maajabu matatu yaliyotangazwa juzi na taasisi ya Seven Natural Wonders ya Marekani ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbunga ya Serengeti na Ngorongoro Crates, Bodi ya Utalii Tanzania TTB iko jijini Berlin nchini Ujerumani ikiongoza makampuni zaidi ya 43 ya utalii katika maonyesho ya kimataifa ya ITB yanayofanyika katika jengo la Mense Berlin.(PICHA NA FULLSHANGWEBLOG)
5 
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akitoa maelezo kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula kulia ni Msaidizi wa Kaimu Balozi Mama Maria Kejo
Kutoka kushoto ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula, Msaidizi wa Kaimu Balozi mama Maria Kejo, Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya Bobby Tours na Mkuu wa utawala ubalozi hapo Bw. Adolf Mchemwa wakiwa katikamkutano huo jana7 
Hili ndilo jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani jijini Berlin.2 
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki katikati akiwa pamoja na Meneja Mkuu wa Masoko wa bodi hiyo Geofrey Meena wakiwa nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kulia ni Kassim Abdallah Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bobby Tours3 
Mmoja wa maafisa wa ubalozi huo akiukaribisha ujumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB ulioongozwa na Mkurugenzi wake Dk. Aloyce Nzuku kulia na Mkuu wa Masoko wa Bodi hiyo Bw. Geofrey Meena katikati ni Kassim Abdallah Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Bobby Tours8 
Kamimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula akipokea majarida na DVD zenye mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania katika nchi za jumuiya ya Ulaya kutoka kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki, mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani jana, kushoto ni Mkuu wa Masoko wa TTB Geofrey Meena na kulia ni Msaidizi wa Kaimu Balozi Bi, Maria Kejo 9 
Kamimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa bodi ya utalii na maafisa wa ubalozi mara baada ya mazungumzo hayo 10 
xHili ndilo banda la Tanzania katika maonyesho hayo likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika jana kabla ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho hayo leo 11 
Mkuu wa Msoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akimueleza jambo Dk. Aloyce Nzuki

WAZIRI WA UTALII ZAMBIA ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA MAONYESHO YA (ITB) BERLIN

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Zambia Mh. Sylvia Masebo akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Ibrahim Mussa akizungmuza wakati waziri huyo alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya (ITB) jijini Baerlin jana katikati ni Katikati ni Balozi Chiti Balozi wa Zambia nchini Ujerumani
1
Waziri wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Zambia Mh. Sylvia Masebo akimueleza jambo Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa Katikati ni Balozi Chiti anayewakilisha nchi hiyo nchini Ujerumani 4 
Dk Wegoro Nyamajeje kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akimuelezea jambo Waziri wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Zambia Mh. Sylvia Masebo kulia wakati waziri huyo alipotembelea katika banda la Tanzania katikati ni Balozi Chiti na Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii 8 
Balozi Ruth Solitei Katibu Mkuu Wizara ya Utalii Kenya kulia akiwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB) Dk. Aloyce Nzuki wakati alipotembelea banda la Tanzania. 7 
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB) Dk. Aloyce Nzuki wa pili kutoka kulia akiwa na maafisa kutoka TANAPA kulia ni John Gara na kutoka kulia ni Maurus Ngairo Ofisa kutoka Mamlaka ya Ngorongoro na Fhadhil Kimambo kutoka (TANAPA) 14 
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii (TTB) Geofrey Meena akizungumza na wageni waliotembelea katika banda la Tanzania
15 
Kulia ni Aileen Mallya na kushoto ni Brenda Mugambi na katikati ni Jane Mbuya maofisa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwa katika maonyesho hayo leo watakuwa na tukio la kuzungumzia utalii wa nchi za Afrika Mashariki wa wageni mbalimbali waliofika katika maonyesho hayo ya (ITB) Berlin.

KIPINDI CHA ‘Ongea na Janet’ CHAPAA NA KUITANGA

$
0
0
Mmiliki na Mweneshaji wa kipindi cha 'Ongea na Janet' Bi. Janet Sosthenes Mwenda.
Sasa ‘Ongea na Janet’ inaonyeshwa katika Dstv kufuatia kuingia nao mkataba.
MO BLOG:Tulishuhudia uzinduzi wa ‘Ongea na Janet’ tukaanza kuona vipindi vikienda hewani hebu tuweke wazi yapi mafanikio uliyopata mpaka sasa..?
JANET: Mafanikio nilianza kuyaona kwenye vipindi 13 tu vya mwanzo ambavyo vilitengeneza ‘Season One’. Nashukuru Mungu ‘Ongea na Janet’ ilijulikana haraka sana, ikapata watazamaji wengi, ‘comments’ nazo zikawa nyingi, ‘changes’ zikawa nyingi nikajikuta kila ninapokwenda siitwi tena Janet naitwa ‘Ongea na Janet’.
Hilo lilikuwa ni fanikio la kwanza kwamba niliondoka kwenye media muda mrefu na niliporudi nikapokewa vizuri kwa hiyo nawashukuru kwanza watanzania wenzangu kwa hilo, nawashukuru sana mashabiki wa Janet kwa kunipa ‘love’ ukweli.
Lakini pia fanikio lingine lilikuja kujitokeza ambalo sikulitegemea kwa kipindi kile lilikuja kama ‘surprise’ kwangu kwani nikiwa sina hili wala line nikapata simu kutoka MNet-Dstv Nairobi wakaniambia kwamba shoo yangu wameipenda na wataichukua, wakati huo nikuwa nimesha ‘apply’ siku nyingi sana mpaka nimesahau.
Wakanipa na ‘amount’ nikakubali wakaniuliza unazo ngapi? Wakati huo ndio nimemaliza ‘Season One’ nikawaambia ziko 13 wakasema wangependa kama zingekuwa 26 nikasema sawa nitakaporudi ‘Season Two’ nitawapatia wakakubali.
Hivyo niliporudi ‘Season Two’ nikawa nimeingia kibiashara zaidi na Dstv wakawa wameni-‘support’ nikaweza kubadilisha set up nzima ya ‘Ongea na Janet’ na wakanipa hamasa zaidi na nikapata nafasi ya kuitangaza nchi yangu kwa na kwa sababu naoneka katika nchi nane (8) tofauti.
Pia nikagundua moja kwa moja kuwa sasa nimeingia kwenye ‘competition’ na watu nane wanaoziwakilisha nchi zao kwa maana ya kwamba Tanzania iko kwenye ‘competition’ ya‘talk show’ na nchi nane za Afrika.
Mashabiki wangu nataka niwaambie kwamba nitajitahidi kuboresha kazi zangu na natamani Talk Show bora East and Central Africa itoke Tanzania.
Mmiliki na Mwendeshaji wa Kipindi cha Ongea na Janet Bi. Janet Sosthenes Mwenda katika moja ya vipindi walivyofanya na Bondia maarufu nchini Tanzania Japhet Kaseba.
MO BLOG: Ni nchi zipi ambazo ‘Ongea na Janet’ inaonekana Afrika..?
JANET:‘Ongea na Janet ‘ inaonekana hapa nyumbani Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), hivyo naweza kusema ‘Ongea na Janet’ bado ina kazi kubwa ya kufanya si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya watanzania wote.
MO BLOG: Baada ya kuingia mkataba na Dstv nini kilifuata..?
JANET: Baada ya kuingia mkataba nao fanikio la kwanza ilikuwa ni kubadilisha ‘set up’ ya kipindi kama nilivyosema na fanikio lingine ambalo lilikuwa ni ndoto yangu ya siku nyingi ni kuanzisha kampuni yangu mwenyewe ambayo itafanya vitu ambavyo natamani kuvifanya na tayari nimeshaifungua.
‘Soon’ itaanza ku-produce yenyewe kipindi cha ‘Ongea na Janet’, lakini sasa hivi tuko kwenye production ya kipindi kingine ambacho ni product ya ‘Ongea na Janet’ kwa hiyo watanzania wakae katika mkao wa kula kwani nitawaletea vipindi vingine viwili japo sita tangaza mimi.
Kwa sasa hivi kampuni yangu inafanya ‘production’ kwa hiyo nimekuwa na Media House, kwa mfano ukija na movie yako tunakurekodia, ukiwa na series zako tunakurekodia, dokumentari yako tunakutengenezea.
Kitu kingine namshukuru Mungu Dstv wamezidi kunifungulia milango kwani wamenifanya kuwa ‘agent’ wao kwa hapa nyumbani Tanzania. Kwa hiyo nimekuwa katikati ya mpishi na mlaji upande wa filamu, series na vipindi kwa hiyo kama kuna mtu sasa hivi ana kipindi anataka kiende Dstv anakileta kwangu, sisi tunakihariri upya, tunakifanyia ‘sub title’ kisha tunakipeleka Dstv.
Ilimradi hiyo kazi iwe ni ya kwake mwenyewe na ameisajili COSOTA.
Kusoma Mahojiano yoteBofya Hapa

TANZANIA YANG’ARA NA VIVUTIO VYAKE VITATU MAONYESHO YA (ITB) BERLIN UJE

$
0
0


Wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakigonganisha glasi za mvinyo wa matunda ya Mananasi uliotengenezwa nchini Burundi wakati wa hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kwenye maonyesho ya utalii ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la Mense Berlin jijini Berlin Ujerumani, Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na mkakati wa Kutangaza utalii wa Afrika Mashariki na mwaka huu ilikuwa na kazi moja ya kunadi maajabu manne ya Afrika yaliyopatikana katika ukanda huu wa nchi za Afrika Mashariki ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mto Nile, Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro Crater huku Tanzania ikiwa kinara kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa maajabu yake matatu ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti na Ngorongoro Crater jambo lililofanya itamkwe mara nyingi miongoni mwa viongozi waliopata nafasi kuzungumzia utalii wa Afrika MasharikiPICHA NA FULLSHANGWEBLOG  
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akipokea tuzo maalum iliyotolewa na iliyotolewa kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Bi Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda katika hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye maonyesho ya (ITB) Berlin jana, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena kulia akiwa na Adolf Mchemwa Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania Ujerumani wakiwa katika hafla hiyo  
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Bi Jesica Eriyo akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo ili azungumze na washiriki wa maonyesho hayo pamoja na wageni waalikwa katika hafla    
Ken Nyauncho Osinde Balozi wa Kenya nchini Ujerumani akizungmza na wageni waalikwa na kueleza ushirikiano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani katika kutangaza utalii   
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Tanzania Bi Maimuna Tarishi akitambulishwa rasmi   
Maofisa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kulia ni Bw. MashauriBrenda Mugambi na Aileen Mallya wakiwa katika hafla hiyo.     
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Chrisopher Mvula kushoto akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki katika hafla hiyo.  
Dk Nyamajeje Wegoro akishauriana jambo na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda katikati ni Bw. Mashauri kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki  
Kikundi cha ngoma kutoka nchini Uganda kikitumbuiza katika hafla hiyo.  
Kikundi cha ngoma kutoka Burundi kikitumbuiza katika hafla hiyo  
Wa kwanza ni Waziri wa Maliasili Uganda B. Maria Mutagamba, Balozi wa Kenya nchini Ujerumani Ken Nyauncho Osinde na Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Bi Maimuna Taarishi wakishiriki kucheza ngoma ya Asili ya Uganda wakati wa hafla hiyo.  
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula kulia akishiriki kucheza ngoma muziki na wageni waalikwa mbalimbali katika hafla hiyo
Viewing all 4405 articles
Browse latest View live