Quantcast
Channel: MRISHO'S BLOG
Viewing all 4405 articles
Browse latest View live

Rap Festival ndani ya Dar Live


SAFARI YA KUJIMBULISHA YA MGOMBEA URAIS WA CCM DKT MAGUFULI

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Rajab Luhwavi akimkaribisha  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  awasalimie wananchi,awashukuru na kujitambulisha kwa wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida. 
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli(kulia) akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Vijijini Dk. Hamisi Kigwangala
 Hussein Bashe ambaye ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la Nzega Mjini akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mjini Nzega. 
 Wananchi wa Nzega wakishangilia mara baada ya kumisikiliza  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  alipomaliza kuwasalimia na kuwashukuru kwa namna walivyojitokeza kumtia moyo,nje ya  za CCM Nzega
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa Nzega kwenye mkutano uliofanyika nje ya ofisi ya CCM wilayani hapo, ambapo aliwaambia Wananchi kuwa amefarijika na mapokezi mazuri na amewaahidi kurudi tena wakati wa kampeni zitakapoanza..
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya  wageni Ofisi za CCM ndani ya mji wa Manyoni  mkoani Singida alipokuwa akipita kuwashukuru Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.
 Wananchi wa Igunga wakiwa na Bango lao wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili maeneno hayo kuwashukuru na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.

Wananchi wa Ikungi wakiwa wamelizunguka gari la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiondoka nzega huku shangwe zikiwa zimetawala kutoka kwa mashabiki mara baada ya kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara
 Wananchi wa Igunga wakimshangila  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea,na pia alijitambulisha kwao.Dkt Magufuli aliwaeleza wananchi hao kuwa ana mambo ya kuwaambia lakini kwa sasa anapita kujitambulisha kwao,kwa sababu wakati wa kampeni bado haujafika,lakini ukifika basi atarejea tena kuzungumna nao kinagaubaga. 
 Wananchi wa Ikungi wakishangilia kwa ujio wa Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.
 Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida. 
Wananchi wa Singida na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida,wakitaka kumuona na kumpongeza  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa mgombea Uraisi wa CCM na pia kumuombea na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kugombea nafasi ya Uraisi
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwashukuru Wananchi wa Singida mjini kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki,walipokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoani humo.
 Mh Mwigulu Nchemba akishangilia jambo mara baada ya kumsikiliza  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida.
 Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akisalimiana na mmoja wa makada wa CCM nje ya ofisi za CCM njini Manyoni Mkoani Singida,mara baada kuwasalimia,kuwashukuru Wananchi waliojitokeza kumpokea na pia alipata nafasi ya kujitambulisha kwa wananchi hao.



MSANII WA BONGO MOVIE AINGIA ACT

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es SalaamNaibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.Msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' akizungumza na waandishi wa habari alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho. 
Msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' akizungumza na waandishi wa habari alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.[/caption] MSANII maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' amejiunga na chama kipya cha siasa cha ACT Wazalendo. Frank amejiunga na chama hicho leo jijini Dar es Salaam akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM). Katika hafla hiyo ya utambulisho kiongozi mwingine ambaye ni Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck pia amejiunga na chama cha ACT Wazalendo na kukabidhiwa kadi za chama hicho. Akiwakabidhi kadi za ACT-Wazalendo, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa leo Makao Makuu ya ACT alisema wamewapokea wanachama hao wapya kwa mikono miwili na wapo tayari kushirikiana nao ndani ya chama hicho. Alisema kuna idadi kubwa ya vigogo kutoka vyama vingine ambao tayari wameomba kujiunga na chama chao na taratibu zinafanywa kutambulishwa. "...tendo hili la leo la kuwakaribisha vijana hawa ni mwanzo wa kuwatambulisha wanachama mbalimbali wakiwemo wabunge na viongozi wa vyama waliojiunga nasi baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Tayari tunao baadhi ya watu waliokuwa wabunge na wameshajiunga nasi na mchakato wa kuwatambulisha unaendelea katika maeneo mbali mbali nchini," alisema Mtemelwa. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano wa ACT Wazalendo. Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano wa ACT Wazalendo.[/caption] Akizungumzia mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, Mtemelwa alisema Julai mosi mwaka huu Chama Cha ACT-Wazalendo kilifungua rasmi pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali zikiweno za Udiwani, Ubunge na Urais. Alisema tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kuchukua fomu na hadi sasa kuna baadhi ya majimbo na kata zina watia azma kuanzia wanne mpaka tisa jambo ambalo alidai ni faraja kwa ACT Wazalendo. "Kati ya majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo tumeshakuwa na waweka azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima na tunaamini mpaka kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote 265 yatakuwa yanawatia azma mbalimbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu," aliongeza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo. Alibainisha kuwa kichama mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi ya udiwani ni julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho ni Julai 31 na kwa nafasi ya Urais mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti Mosi, 2015. "Kwa ngazi ya Taifa Halmashauri kuu itakutana Agosti 13 kwa ajili ya kuteua jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu. Agosti 13, Mkutano mkuu utamchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama cha ACT Wazalendo katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.""Hivi karibuni tumepokea taarifa kutoka katika miji ya Tarime na Rorya Mkoani Mara kuwa kuna watu wanapita na kutangaza kuwa Chama chetu kimezuiwa kushiriki Uchaguzi kwa muda wa miezi sita. Tumebaini lengo la upotoshaji huu ni kuwakatisha watanzania tamaa juu ya ukuaji wa Chama Cha ACT-Wazalendo pamoja na dhamira yake nzuri ya kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere. "Tunawataarifu wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama hakitakuwa tayari kuona sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita bila kupingwa," alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

BHALALUSESA ASISITIZA UMUHIMU WA UMAHIRI KATIKA TEHAMA

$
0
0
IMG_8834
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (hayupo pichani) kufungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo.
IMG_8915
Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalusesa wakati akifungua rasmi kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo. Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.
Alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akifungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa alisema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na hivyo wakufunzi lazima wawe mahiri.
"Duniani kote, sekta ya uchumi, fani mbalimbali, taasisi na hata mifumo ya maisha yanategemea sana matumizi ya Tehama kwa sasa. Kadhalika, maendeleo makubwa katika Tehama yamebadili namna mambo yanavyofanyika,” alisema.
Alisema kwa kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya kutosha ni vyema walimu kuwa na umahiri unaotakiwa kwani Tehama inachangamoto nyingi zinazotakiwa kuangaliwa ili kuweza kuitumia ipasavyo kuleta mabadiliko katika jamiii.
Aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanapitia muswada huo kwa makini na kujazia maeneo yote ambayo wataalamu wameshindwa kumaliza na kusaidia kuweka mtaala huo vyema kwa mafunzo.
Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa kuimarisha uelewa kwa wanafunzi na wakufunzi vyuo vya walimu ili kuboresha matumizi ya Tehama katika mafunzo hasa masomo ya sayansi limeshirikisha wataalamu mbalimbali na kuendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na watu wa China.
Alisema kwamba serikali inatambua kuwa Tehama inaweza kutumika vyema katika kubadili na kuboresha mfumo wa elimu Tanzania.
Aidha alisema Sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatambua umuhimu wa Tehama katika kuboresha viwango vya elimu nchini Tanzania.
Alisema moja ya malengo ya sera ni kuonesha mahitaji halisi ya Tehama nchini katika upande wa wataalamu na vifaa ili kufanikisha utoaji wa elimu hata ya masafa katika ngazi zote.
Kongamano hilo ni moja ya mradi wa China Funds in Trust Project (CFIT) wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua tehama na kuitumia.
Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu vitaingizwa.
IMG_8909IMG_8842
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu wakati kongamano hilo likiendelea mjini Bagamoyo.
IMG_8843IMG_8831
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kushoto) akijadili jambo na mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (katikati). Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
IMG_8826
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kulia), akifurahi jambo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kushoto) mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
IMG_8928
Mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (walioketi wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo inayomalizika leo mjini Bagamoyo.

WASIMAMIZI, WAHARIRI NA WADADISI WA UTAFITI WA AFYA YA MAMA, MTOTO NA MALARIA WA MWAKA 2015,WAPEWA MAFUNZO

$
0
0
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi,wahariri na wadadisi wa utafiti wa afya ya mama na mtoto na Maralia yanayofanyika kwa siku 36 katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.

Baadhi ya wauguzi wanaoshiriki mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Takwimu ,Ephraim Kwesigabo akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Zanzibar Halima Maulidi Saleh akiwa na ,Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Andrewleon Qweker (katikati) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizindua matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Afya ,Zanzibar Halima Maulid Saleh  matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Andrewleon Qweker matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab  matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu  Ephraim Kwesigabo matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wauguzi kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

LISTEN TO ERICA LULAKWA’S BRAND NEW SONG “DUNDIKA”

$
0
0
maxresdefault
Debut Album "Piga Moyo Konde" is out! On Itunes http://itunes.apple.com/album/id10046...
Dundika is the 2nd Song released from this Album. Listen free on Spotify and Tidal. If you like the music, I would truly appreciate your support in writing a review or sharing links to iTunes or Google Play on social media.
Listen to her music on you tubebelow here.

DIAMOND PLATNUMZ NA MASANJA WATUA MOSHI KUWEKA HISTORIA LEO

$
0
0
 Mwanamuziki Naseeb Abdul almarufu kama Diamond Platnumz akisalimia warembo baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro International Airport (KIA).



Shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 linafanyika usiku wa leo katika viwanja ya Kili Home Resort kuanzia saa mbili usiku likiambatana na burudani za muziki wa kizazi kipya ambapo wasanii mbalimbali watatumbuiza akiwemo Diamond Platnumz na burudani ya Uchekeshaji kutoka kwa Masanja Mkandamizaji. 

TOP JOBS FOR THIS WEEK

$
0
0

TOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU KUTOKA MAREKANI ATUA NCHINI

$
0
0
King Nahh

King Nahh akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo

 Akikabidhiwa shada la mauwa uwanjani hapo
King Nahh akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanjani hapo
 Meneja wa King Nahh akisisitiza jambo kwa wanahabari

 King Nahh akicheza ngoma ya utamaduni
 King Nahh akizungumza na wananchi katika viunga vya uwanja wa ndege
 Akiwa amepozi na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo

 Akisaini kitabu cha wageni katika Supermarket ya Uchumi
 Akimlisha keki mmoja kati ya wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
 Akilishwa keki na msanii nyota wa filamu, Iluminata Alfonce 'Dotnata'
 Akikabidhiwa 'token' na Meneja wa Uchumi Supermarket kwa ajili ya kununulia bidhaa katika kipindi atakachokuwa nchi, pembeni yake ni mratibu wa kongamano Cynthia Henjewelle
 Akitaniana na wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
 Akijichagulia bidhaa

Na Mwandishi Wetu
MTOTO  mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri  wa kujijengea uwezo wa kujiamini  anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani,  Lonnie Hudson  maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua  jijini Dar es Salaam , leo.

King Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson  ambapo wapo nchini kwa mwaliko wa  taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partner.
Kesho mtoto huyo atafanya  kongamano kubwa  la watoto na wazazi  katika Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za  watu ambao wamekata  tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini katika maamuzi.

“Najisikia furaha kuja Tanzani. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa. Hususani  kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza kubadili hisia zao, kujiamini na  kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,” alisema.

King Nahh aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana na kuishia kulaumu  matatizo na vikwazo bila kutafuta suluhu ya matatizo yao.

“Kila mtu analaumu. Wa kwanza atalaumu, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano mpaka wa sita. Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa hawezi kitu. Ila ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu unaweza kufanya. Jamii ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na kushangaza watu waliokwenda kumlaki.

Mkurugenzi wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira kubwa ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii hasa watoto ili waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.

“King Nahh ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na  kipawa  alichonacho. Wazazi wawalete watoto kesho  Urafiki,  ili waweze kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza mtoto huyu kuanzia saa tano asubuhi,”alieleza Henjewele.

DKT MAGUFULI AREJEA JIJINI DAR BAADA YA KUJITAMBULISHA MIKOA KADHAA,APOKELEWA KWA KISHINDO

$
0
0
 Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Chalinze (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodomaakitokea Mkoani  Dodoma. 
PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP
 Wakanazi wa Bagamoyo wakimsikiliza Dkt Magufuli wakati alipokuwa akijitambulisha kwao
 Mkazi wa Bagamoyo akifurahia jambo
 Wananchi wakimshangilia Dkt Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa akijitambulisha kwao hapo mjani mjini Bagamoyo

  Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Chalinze (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodomaakitokea Mkoani  Dodoma.
 Wananchi wa Chalinze wakiwa wamelizunguka gari la Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Kiwangwa  alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimshangilia kwa mayowe Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Kiwangwa alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

 Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimsikiliza Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma. 
  Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
   Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete pamoja na  Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia jambo mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini meneno ya Dkt Magufuli
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Rajab Luhwavi akizungumza jambo na Mh.Ridhiwani Kikwete
 Dkt Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Bagamoyo mapema jana

Angalia Nyumbani Na Diaspora na David Kyungu-TBC1

Mahojiano na Charles Magali ndani ya Washington DMV

$
0
0
Charles Magali akiwa ndani ya Kilimanjaro Studio zinazomilikiwa na Vijimambo Radio, Kwanza Production na NesiWangu Media
Ijumaa ya Julai 24, 2015, mwigizaji na mwimbaji wa muziki nchini Tanzania Charles Magali alipata fursa ya kutembelea studio zetu zilizopo Beltsville Maryland. Hapo akazungumza nasi kwa ufupi
Karibu umsikilize akihojiwa na Mbunifu na Mtayarishaji wa kipindi hiki Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio

WATIA NIA WA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI KUPITIA CCM WAJINADI MBELE YA WAJUMBE KATA YA MAWENZI

$
0
0
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini Priscus Tarimo akijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mawenzi wakiwasikiliza wagombea.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Edmund Rutaraka akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
Baadhi ya wajumbe katika kata ya Mawenzi.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Patrick Boisafi akiomba kura mbele ya wajumbe wa kata ya Mawenzi,
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini Chief Omary Mwaliko akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata a Mawenzi.
Omary Mwaliko akipongezwa na wanachama a chama hicho mara baada ya kutoa maelezo yake katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Hindu Mandal.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha aijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Msohi mjini,Athuman Ramole maarufu kama Buni akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata ya  Mawenzi.
Baadhi ya wagombea wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi Donatha Mushi mara baada ya zoezi la kujinadi mbele ya wajumbe kumalizika.
Watia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini wakiwa katika gari moja wakielekea katika kata nyingine kuomba kura.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

CHADEMA MOSHI MJINI WAMPITISHA JAFARY MICHAEL KUWANIA UBUNGE WA JIMBO HILO.

$
0
0
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi mjini wakiwa katika mkutano maalumu wa kumchagua mtia nia atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge anayemaliza muda wake,Philemoni Ndesamburoakizungumza wakati wa mkutano huo.
Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi mjini,Joel Makwaia akizungumza katika mkutano wa Chadema alipoalikwa kukiwakilisha chama chake.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Moshi mjini,Leonard Buberwa akizungungumza akati wa mkutano wa kumpata mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini.
Watia nia katika nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini,Basil Lema,(kushoto) Jafary Michael (katikati) na wakili wa kujitegemea ,Elikunda Kipoko  wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza.
Mbunge wa iti maalumu,Chadema,Lucy Owenya alikuwa ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Ubunge aliyejitokeza kutetea kiti chake.
Wajumbe wa mkutano wakishangilia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Msimaizi wa Uchaguzi ,katibu wa baraza la wanawake mkoa wa Kilimanjaro ,Helga Mchomvu akitangaza matokeo katika uchaguzi huo ambao mgombea Basil Lema aliamua kujitoa kabla ya kura kupigwa.
Mtia nia aliyetangazwa mshindi Jafary Michael akiwa na mkewe katika ukumbi wa Umoja Hotel ambako uchaguzi huo ulifanyika.
Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo aliyepata kura 9 ,Elikunda Kipoko akizungumza na kuwashukuru wajumbe kwa wale waliompigia kura .
Jafary Michael aliye chaguliwa na Chadema kupeperusha Bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba katika kuwania kiti cha Ubunge jimbo la Moshi mjini.
Michael aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,akimtambulisha mkewe mbele ya wapiga kura.
Mgombea wa nafasi ya viti maalumu ,Lucy Owenya akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumuamini na kumchagua tena kupeperusha bendera ya chama hicho kupitia viti maalum.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Basil Lema aliyekuwa miongoni mwa wagombea kabla ya kujitoa akizungumza katika mkutano huo mara baada ya Jafary Michael mkutano huo kupitisha jina lake kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama hicho katika jimbo la Moshi mjini.  

Madaktari Diaspora kutoka Marekani wakitowa Huduma ya Elimu kwa Wanafunzi wa Chuo cha Eilimu ya Afya Kuhusiana na Saratani ya Matiti na Meno.Wakiwa Zanzibar

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai, akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari Diaspora kutoka Washington walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Washington  wakali walipofika katika Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar walipofika hapo kutowa Elimu ya Afya ya Saratani ya Matiti na Mano, wakiwa Zanzibar kwa uwenyeji wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washinton Ndg Iddi Sandaly akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari 17 Diaspora, waliofika Zanzibar kutoa Tiba ya Maradhi ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Meno akitowa maelezo wakati walipofika katik Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar, na kutowa Elimu ya kutambua Saratani ya Matiti kwa Kinamama. na kutowa huduma ya uchunguzi wa Meno.
Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Womens Cancer Awereness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko Afrika.    

Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Womens Cancer Awereness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko Afrika.
Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakimsikiliza Dr Ify akitowa maelezo na kuwatambulisha Madaktari Diaspora aliofuatana nao. 
Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa Elimu ya tambua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa wanafunzi hao wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar,
Dr Ify akitowa mada kuhusiana na Saratani ya Matiti kwa Wanafunzi wa Chuo hicho hutoa Elimu ya Udaktari wa aima mbalimbali chuoni hapo.
Dr Ify akionesha Mashine ya kupimia Saratani ya Matiti ya Kisasa inayoitwa MamaGram hutumika kucunguza viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanachuo hao wakati akitowa Elimu ya Saratani ya Matiti jinsi ya kumgundua Mwanamke mwenye matatizo hayo. 
             Wanafunzi wa Chuo hicho wamepata fursa ya kuuliza mswali wakati wa Mafunzo hayo.
Mmoja wa Madaktari hayo akitowa mfano hai kutokana na matatizo ya Saratani ya Matiti, kwa Wanachuo hao. 
Daktari wa Meno Bi Queenate Ibeto akitowa elimu ya kutunza meno na kinga ya mane kwa Wanafunzi hao jinsi ya kuyatunza meno. wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho. 
Daktari wa Meno Venessal Quitero akionesha moja ya tiba ya kunusuru meno kwa wanafunzi hao wakati wakitowa Elimu ya Utunzaji wa Meno na tiba yake.
Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar akionesha mafunzo ya utunzaji wa Meno kwa vitendo jinsi ya kupiga msuwaki inavyotakiwa kuweza kuimarisha meno kuwa imara 
Dr Queenate Ibeto akionesha mfano ya vitendo kwa mmoja wa mnafunzi wa Chuo hichi jinsi ya utumiaji wa msuaki katika kupiga kwa Wanafunzi hao, wakati walipofika kutoa Elimu ya Afya kwa Wanafunzi wa Chuo hicho Mombasa Zanzibar. 
Profesa Hailu na Dr Quintero wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwakilishwa kuhusiana na Saratani ya Matiti na Tiba ya Meno, kwa Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar Mombasa wakati walipofika katika Chuo hicho wakiwa Zanzibar kwa ajili ya kutoa Tiba ya Saratani ya Matiti Ugonjwa wa Kisukari na Meno.
Dr Quintero ni mtaalamu ya Magonjwa ya Meno akifafanua moja ya swali lililoulizwa na Wanafunzi wa Chuo hicho. 
Mwanafunzi wa chuo hicho akiuliza swali kuhusiana na baadhi ya Wananchi meno yao huwa na ukungu mweusi kwa wataalam hao
Madaktari wa Diaspora wakigawa misuwaki na dawa za meno kwa wanafunzi hao baada ya kutowa Elimu chuoni hapo,
Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa wanafunzi hau jinsi ya kumgundua mwanamke mwenye matatiti ya Saratani ya Matiti wakati wakifanya mafunzo hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya Afya ya binadamu,
Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa wanafunzi hau jinsi ya kumgundua mwanamke mwenye matatiti ya Saratani ya Matiti wakati wakifanya mafunzo hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya Afya ya binadamu,  
Dr Ify  akitowa Elimu ya Vitendo kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Mwanamke akitowa mafunzo hayo ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Dr Ify akitowa Elimu ya Vitendo kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Mwanamke akitowa mafunzo hayo ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar kulia Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai,
Madaktari Diaspora wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar baada ya kutoa Elimu kwao,
DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.
DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.
DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.
Madaktari wa Diaspora wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakiwa nje ya jengo la Chuo hicho katika Skuli ya Sekondari ya SHAA Mombasa Zanzibar.
Picha na OthmanMapara.Blog  Zanzinews.Com

MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI NCHINI KWA NUSU YA KWANZA YA MWAKA 2015…

$
0
0



 By Willliam Kaijage
UTANGULIZI (PREAMBLE)
Mwanzoni mwa mwezi wa 7 ndio nusu ya mwaka. Zinakuwa zimepita siku 182 (au 183 kwa mwaka mrefu) na kubaki siku 182.
Yafuatayo ni matukio makubwa ya muziki wa dansi kwa nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2015


BENDI MPYA
Tarehe 31-Jan-2015, BMM Classic Band, ilizinduliwa katika ukumbi wa BMM Mwenge, opposite TRA.
Tarehe 21-Feb-2015,  JJ Band yazinduliwa katika ukumbi wa. JJ Band ni bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe Resort.
 Tarehe 06-Mar-2015 (Ijumaa), Ruby Band ilitambulishwa rasmi katika ukumbi wa Coco Beach Pub ambapo pia ilizindua video ya wimbo mpya wa “Noma”.
Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), Stars Band yazinduliwa katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo inaongozwa na mwanamuziki Aneth Kushaba aka “AK47” aliyekuwa Skylight Band. Meneja wa bendi ni mpiga drums James Kibosho.

UZINDUZI WA ALBUM MPYA
Mpaka sasa (zaidi ya nusu mwaka) hakuna album yoyote mpya hata moja iliyozinduliwa.

KILI MUSIC AWARD
Tarehe 23-Mar-2015, Kililimanjaro Music Award 2015 yazinduliwa rasmi
Tarehe 25-Apr-2015, Academy ya Kili Music Award yakutana kuchagua majina ya washiriki wa kila kipengele.
Tarehe 29-Apr-2015, majina ya washiriki wa kila kipengele yatangazwa rasmi
Tarehe 13-Jun-2015 (Jumamosi), sherehe za washindi wa Kili Music Award 2015 zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 6  vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
1. Bendi Bora ya Mwaka- FM Academia
2. Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi-Jose Mara (Mapacha Watatu)
3. Rapa Bora wa Mwaka Bendi- Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo wa Kiswahili Bendi- ”Wale Wale” (Vijana Ngwasuma)
5. Mwimbaji Bora wa Kiume Bendi- Jose Mara (Mapacha Watatu)
6. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo Bendi-Amoroso Sound

NB: Mwaka huu hakukuwa na Mwimbaji Bora wa Kike Bendi

WANAMUZIKI WALIOFARIKI
Tarehe 04-Jan-2015 (Jumapili), mwanamuziki wa Flowin aka “Kachumbari” aliyekuwa mpiga drums na tumba wa Chuchu Sound afariki dunia.
Tarehe 30-Jan-2015, mwanamuziki Peter Kanuti afariki dunia kwa ajali ya gari akiwa Zanzibar. Huyu anatokea familia ya wanamuziki Gaspar Kanuti, Fred Kanuti na Joseph Kanuti.
Tarehe 28-Feb-2015, mwanamuziki, mwanasiasa, mwanajeshi mstaafu, mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, Mkurugenzi wa kundi la sanaa za maonesho la Tanzania One Theatre (TOT Plus) Captain John Damian Komba afariki dunia
Tarehe 16-Apr-2015, mwanamuziki Joseph Chigwele “Che” Mundugwao afarikia dunia.
Mwanamuziki Mutombo Lufungula “Audax” mmoja ya waanzilishi na wamiliki wa bendi ya Maquis du Zaire (ambayo baadaye ikaitwa Maquis Original) afariki dunia alfajiri ya alhamis tarehe 23-Apr-2015 na kuzikwa Jumapili ya tarehe 26-Apr-2015 katika makaburi ya Kinondoni.
Tarehe 17-Jul-2015 (Ijumaa), mwanamuziki Ramadhan Ally Masanja aka “Banza Stone” afariki dunia siku ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Azikwa Jumamosi tarehe 18-Jul-2015 sikuu kuu ya Idd Mosi (Eid al Fitr) katika makaburi ya Sinza.

MATUKIO MENGINE MAKUBWA
Tarehe 18-Jan-2015 (Jumapili), Ali Choki apanda jukwaa la Twanga Pepeta siku Twanga walipokuwa wakitumbuiza Leaders Club na kusalimia kisanii. Tukio hili halijawahi kutokea tangu Ali Choki alipohama Twanga Pepeta mwaka 2008 na kwenda kujiunga na TOT Plus.
Ndani ya siku 3 kuanzia 24-26 January 2015, Wadau wa Muziki wa dansi chini ya uratibu wa admin wa BONGO DANSI Deo Mutta Mwanatanga wafanikisha harambee na zoezi la kumrudisha Dar-es-Salaam mwanamuziki Banza Stone aliyekuwa amekwama mjini Tunduma huku akiwa anaumwa baada ya matatizo yaliyoitokea bendi ya Rungwe aliyoenda nayo huko.
Tarehe 24-Jan-2015 (Jumamosi), tamasha linaloitwa TIGO KIBOKO YAO Concert lafanyika Leaders Club. Bendi za muziki wa dansi zilizoshiriki ni Msondo Ngoma, Mlimani Park Orchestra, Christian Bella & Malaika Music Band, Yamoto Band. Kila bendi ilipiga kwa dakika 45.
Tarehe 25-Jan-2015 (Jumapili), tamasha la miaka 10 ya CDS lafanyika TCC Chang’ombe na kushirikisha bendi za muziki wa dansi za Msondo Ngoma, Mapacha Watatu, Malaika Music Band na FM Academia. Kuna uwezekano tamasha hili likawa linafanyika kila mwaka.
Tarehe 30-Jan-2015, Ali Choki na Mama Asha Baraka wapatanishwa rasmi chini ya usuluhishi uliofanywa na Global Publisher.
Tarehe 07-Feb-2015 (Jumamosi), tukio la “Miaka 16 ya Luizer Mbutu” ndani ya Twanga Pepeta lafanyika Mango Garden.
Tarehe 28-Mar-2015 (Jumamosi), wafanyika mpambano kati ya FM Academia na Twanga Pepeta katika ukumbi wa Escape One.
Tarehe 08-Apr-2015, Ally Choki na Super Nyamwela watangazwa rasmi kujiunga (kurejea) Twanga.
Tarehe 18-Apr-2015 (Jumamosi), Christian Bella afanya tukio la “Usiku wa Masauti” ndani ya ukumbi wa Escape One. Christian Bella atumia tukio hilo kutambulisha/kuzindua audio na video ya wimbo wake mpya wa “Nashindwa”.
Tarehe 25-Apr-2015 (Jumamosi), show ya kwanza ya Ally Choki na Super Nyamwela baada ya kurejea Twanga Pepeta yafanyika Mango Garden.
Tarehe 25-Apr-2015 (Jumamosi), kundi la Les Wanyika kutoka Kenya latumbuiza katika kiwanja cha Escape One.
Tarehe 26-Apr-2015, Bendi ya Cuban Marimba watunukiwa nishani ya Muungano kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya ikulu. Waliopokea nishani kwa niaba ya bendi ni Waziri Nyange (mpiga solo) na Mzee Juma Sangura (mpiga bass).
Tarehe 08-May-2015 (Ijumaa), Mashujaa Group wazindua ukumbi wao wa Mashujaa Lounge ambao zamani ulikuwa unaitwa Business Park uliopo maeneo ya Victoria, Dar-es-Salaam. Katika tukio hilo, Mashujaa Band imetumia nafasi hiyo pia kutambulisha wanamuziki wawili wapya Roggart Hegga Katapila na Dady Dipirone “Rais wa Masauti ya Chini”. Pia Mashujaa Band walitambulisha nyimbo 2 mpya. Ikumbukwe pia kuwa Mashujaa Group mwaka huu wamefanikiwa kuanzisha radio ya Mashujaa FM mkoani Lindi.
Tarehe 24-Jun-2015, mwanamuziki Ramadhan Masanja aka “Banza Stone” alizushiwa kifo baada ya kuumwa muda mrefu. Hii ni moja ya mara nyingi sana mwanamuziki huyo kuzushiwa kifo.
Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika siku ya Idd Mosi (Eid al Fitr) katika ukumbi wa TCC Chang’ombe kwa kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment.

Madaktari wa Diaspora Wakabidhi Msaada wa Dawa za Magonwa ya Binaadamu

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Jidawi akizungumza na Madaktari Diaspora kutoka Washington walipofika Afisini kwake kwa kujutambulisha ujio wao Zanzibar walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Washington wakiwa chini ya uenyeji wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),wakiwa Zanzibar wametoa huduma ya kucheki waginjwa wa Kisukari na Meno na kutoa Elimu ya Afya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar.   
Katibu Mkuu Dr Jidawi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Madaktari hao walipofika Afisini kwake wakiwa na Ujumbe wa Watu 17 wakiwemo Madaktari wa Saratani ya Matiti kwa Kina mama, Kisukari na Meno.
Madktari wa Diaspora kutoka Washington wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar walipofika Afisi kwake 
Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai wakiwa na wenyeji wao wakifuatilia maongezi na Dr Jidawi walipofika kuwatambulisha madaktari hao. kupitia Jumuiya ya Watanzania Washington
Mkuu wa Ujumbe huo,Rais wa Jumuiya ya Wanawake (Africa Womens Cancer Awareness Assciation) Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa shukrani kwa ushirikiano waliopata wakiwa Zanzibar katika kufanikisha malengo ya kutowa huduma kwa Jamii ya Tiba ya Saratani ya Matiti na Elimu ya vitendo kuhusiana na Viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanafunzo wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Mkuu wa Ujumbe huo Rais wa Jumuiya ya Wanawake (Africa Womens Cancer Awareness Assciation) Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa shukrani kwa ushirikiano waliopata wakiwa Zanzibar katika kufanikisha malengo ya kutowa huduma kwa Jamii ya Tiba ya Saratani ya Matiti na Elimu ya vitendo kuhusiana na Viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanafunzo wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Daktari wa Meno akuzungumza wakati wa mkutano huo na Katibu Mkuu Wizaya ya Afya Zanzibar walipofika Afisini kwake kujitambulisha. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Saleh Mohammed Jidawi akipokea msaada wa Dawa za Binaadamu kutoka kwa Daktari  Jummy Amuwo kwa niaba ya Madaktari wa Dispora kutoka Washington  wakiwa Zanzibar  mualiko wa Jumuiya ya Watanzania Washingto, akishuhudia Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid, makabidhiano hayo yamefanyika katika Afisi za Wizara ya Afya Zanzibar
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washington Ndg Iddi akiungezani na Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid baada ya makabidhiano ya madawa ya Binaadamu yaliotolewa na Madaktari Diaspora Washington. hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar. 
 Wakipongezani kwa ushirikiano waliouonesha kwa mapokezi waliopata wakipongezana baada ya hafla hiyo.


Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Wizara ya Afya Zanzibar, baada ya hafla ya kukubidhi msaada wa dawa
Madaktari Diaspora wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar nje ya Jengo Wizara ya Afya Zanzibar baada ya hafla ya kukabidhi dawa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Jidawi.
Picha zote na OthmanMapara.Blog. Zanzinews.Com. 

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIANA NA TANZANIA KUINUA ELIMU

$
0
0
IMG_8896
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
IMG_8887
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.
IMG_8817
Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.
Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.
Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.
“Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.
Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.
IMG_8793
Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
“Leo tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document (kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.
IMG_8775
Alifafanua kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.
Naye kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania na Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi .
Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu na ubora wa walimu.
Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama.
Alisema mradi huo utasaidia kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.
Profesa Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni matarajio yao kwamba wakishafikisha hati hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.
IMG_8849
Pichani juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.
IMG_8798
IMG_8821
IMG_8787
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.
IMG_8842

WAJASILIAMALI 150 WAPATIWA MAFUNZO MOSHI.

$
0
0
Baadhi ya Wawezeshaji katika mafunzo yaWajasiliamali 150 yanayofanyika katika chuo cha Ufundi Veta mkoa wa Kilimanjaro.

Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki na Kusinin(ESAURP) Prof,Ted Maliyamkono akzungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajasiliamali  wadogo wa mkoa wa Kilimanjaro yanayofanyika katika chuo cha VETA Moshi.
Badhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tano.
Mjumbe wa  Bodi ya Taasisi ya fedha ya FSDT ,Erick Masinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wajasiliamali hao.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Lembris Kipuyo akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha kurasimisha biashara zo ili wapate mkopo na kukuza Biashara.
Prof Maliyamkono akitoa neno la Shukrani.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo,wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo.
DC Kipuyo akizungumza na wanahabari mara baada ya kufungua mafunzo hayo.
DC Kipuyo akifanya mahojiano na mmoja wa wanahabari .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI KATIKA KESI YA MIRATHI YA MWANDISHI WA HABARI MKONGWE NCHINI.

$
0
0
Viewing all 4405 articles
Browse latest View live